Friday, October 3, 2014

SHIGONGO AZINDUA VITABU VYAKE VIPYA MAREKANI

Vitabu viwili vya Eric Shigongo alivyozindua nchini Marekani juzi.
Eric Shigongo akihojiwa na Shaka Ssali (kulia) katika kipindi cha Straight Talk Africa kabla ya uzinduzi huo.
MKURUGENZI Mtendaji wa Global Publishers, Eric James Shigongo amezindua vitabu vyake viwili vipya vya namna ya kuondokana umaskini vyenye majina ya 10 Laws-How to Move From Poverty to Prosperity na 26 Secrets- How to Defeat From Enemies and Make Millions of Dollars.
10 Laws-How to Move From Poverty to Prosperity.
Shigongo alizindua vitabu hivyo vya ujasiriamali alipokuwa akihojiwa na Kituo cha Runinga cha Voice of America (Voa) kwenye Kipindi cha Straight Talk of Africa nchini Marekani juzi.
26 Secrets- How to Defeat From Enemies and Make Millions of Dollars.
Kwa mujibu wa Shigongo vitabu hivyo vitakuwa vikiuzwa duniani kote ili kuikomboa jamii kwenye wimbi la umaskini.

1 comment:

Anonymous said...

Fact: Masikini wengi hawajui kusoma wala kuandika, je hao utawaidiaje?
Na pesa ya kununulia hivyo vitabu wapate wapi?
Kama utajiri ni kuandika habari zisizo na udhibitisho then ni rahisi, just make up stories about 'famous people'