Na Baraka Mbolembole
Wachezaji sita wa timu ya Stand United wameondoka katika timu hiyo na kurudi ‘ majumbani’ mwao baada ya hali mbaya katika timu hiyi. Hakuna huduma nzuri katika kambi ya timu hiyo, maradhi ni shida, huku wachezaji wanaopata majeraha wakitibiwa kwa Panaldo. Patrick Mrope ni mmoja wa wachezaji sita ambao wameamua kuachana na timu hiyo na kufikia tarehe 26, Mwezi huu mchezaji atakuwa huru kwa sababu atafikisha miezi mitatu bila kulipwa mshahara wake.
“ Mlinzi wa kulia ambaye ana kipaji kikubwa na uwezo wa kupiga mashuti, Kulwa ameondoka na kurudi kwao Morogoro baada ya maisha kuwa magumu katika kikosi cha Stand . Pastory Patrick ‘ Pato’ mshambulizi ambaye alikuwa na mchango mkubwa wakati timu hiyo ikipanda daraja, yeye ameumia bega lakini mpaka sasa hajapewa huduma yoyote ya kitabibu. Hajapigwa X’ray badala yake daktari wa timu amekuwa akimpatia vidonge vya Panadol”
“ Dk, hana vifaa wala hana nguvu ya kusema kwa sababu akifanya hivyo ataondolewa” anasema, Mrope mchezaji wa zamani wa Ashjanti United, Manyema Rangers, CDA Dodoma , Coastal Union, ambaye ameshindwa kucheza katika timu hiyo ya Shinyanga. Stand inaendeshwa ‘ kihuni-huni’ kwa maana kwamba timu hiyo inaendeshwa kama timu ya Mtaani na si yenye hadhi ya ligi kuu.
Hiki ni moja kitanda kinacholaliwa na wachezaji wawili………………
“ Nimecheza mpira katika timu nyingi lakini ndani ya Stand United nimekutana na maisha ambayo huwezio kuamini. Sijawahi kuona maisha ya wachezaji yalivyo magumu kama pale ( Stand). Mara baada ya kufika katika timu hiyo, siku ya tatu tu nilianza kuona dalili mbaya. Tulifikia gesti na tulikaa hapo kwa siku chache. Tulipopolekwa katika kambini, ilibaki kidogo nichukue begi langu niondoke kurudi nyumbani. Mazingira ya kambi ni mabaya sana, chumba kimoja tulilazimika kulala wachezaji tisa, tisa, wakati huo huo kitanda kimoja cha futi 3 tukawa tunalala wachezaji wawili, wawili. Wengine wanaweka magodoro chini na kulala”
anaongeza Mrope ambaye pia anawaambia mashabiki wa soka wapunguze kuwatukana wachezaji wa timu yao wanapokuwa uwanjani kwa sababu maisha yao kabla ya kuingia uwanjani yamejaa ‘ mashaka’ makubwa.
Hii ndo ‘Breakfast’ ya wachezaji wa STAND UTD…….Kikombe cha Chai ya rangi pamoja na maandazi matatu…..
“ Kama timu hiyo itapata mahitaji yanayokidhi ni moja ya timu nzuri kwa sababu kuna wachezaji wengi wazuri na wana vipaji vikubwa. Mechi na Simba wachezaji walicheza kwa kiwango cha juu kwa sababu walihitaji kuonekana, hii ni mechi ambayo wachezaji vijana wanapenda kuzicheza. Sitarudi hata kama watanilipa mshahara wangu kwa sababu tayari nimeamua kukaa kando. Nimejitoa ‘ mhanga’ kuzungumza mambo hayo hadharani ili vijana wngine waliopo katika timu wapate unafuu.
Kuna Warundi wawili katika timu ile, ukweli wanateseka kutokana na maisha wanayoishi pale, kama viuongozi wa timu hiyo wapo, naomba wawapatie nauli warudi nyumbani kwao. Hadi jana wachezaji sita wameoondoka katika timu hiyo na wanacheza kufikia wachezaji kumi ( 10-13) katika siku chache zijazo kama uongozi hautasimama na kushughulika na matatizo hayo ndani ya timu” anasema, mshambulizi huyo wa zamani wa Polisi Dar es Salaam.
Credit:Shaffih Dauda
No comments:
Post a Comment