Mwanasiasa mkongwe nchini, Dk. Chrisant Mzindakaya
Mwanasiasa mkongwe nchini, Dk. Chrisant Mzindakaya, amewashauri wanaokusudia kuandamana nchi nzima kutopoteza nguvu na muda kwa kuwa uamuzi wote kuhusu Katiba mpya, utaamuliwa na wananchi kupitia kura ya maoni.
Dk. Mzindakaya, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC), alikuwa akizungumzia maamuzi ya Bunge Maalum la Katiba lililohitimisha shughuli zake mjini Dodoma wiki iliyopita.
"Waliosema Katiba itokane na wananchi, basi sasa wawaache waamue bila kuwaburuza...Vijembe havisaidii bali tunapaswa kuijenga nchi yetu kwa pamoja,” alisema.
Alisema Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, wameamua kubakia wamoja badala ya kutengana.
Dk. Mzindakaya alisema wajumbe wa bunge hilo walitumia busara kuepusha hatari ya kuvunjika kwa Muungano ulioasisiwa na hayati Mwalimu Julius Nyerere na Rais Abeid Amani Karume, wa Zanzibar.
Alifafanua kuwa lengo la pendekezo la Serikali tatu lilikuwa ni kuuvunja Muungano ambao umeujengea taifa la Tanzania heshima kubwa duniani.
“Waliotarajia mpasuko kwa kuvuruga mchakato wa kupata Katiba mpya hawakufanikiwa. Wabunge wameonyesha ukomavu wa kisiasa. Waliosema katiba itokane na wananchi sasa waache kuwaburuza kwa kudai maandamano," alisisitiza Dk. Mzindakaya.
Alisema baadhi ya watu wa nje wanaojidai kuwa magwiji wa demokrasia, wamekuwa wakifanya kila hila kuvuruga mchakato wa Tanzania kujenga demokrasia ya kweli.
“Kamati za Bunge Maalum zilijadili kwa kina maboresho ya vipengele mbalimbali katika Katiba iliyopendekezwa kama uchumi, masuala ya umiliki wa ardhi, ushirkishwaji wa wanawake katika ngazi mbalimbali za maamuzi na utendaji, haki za makundi yote na uongozi shirikishi pasipo ubaguzi," alisema.
Aidha, Dk. Mzindakaya amempongeza Rais Jakaya Kikwete, kwa kuanzisha mchakato wa nchi kupata Katiba mpya.
Kadhalika, ameungana na pendekezo la Waziri Mkuu, Mizengao Pinda, kwamba Katiba mpya ipatikane kabla Rais Kikwete hajaondoka madarakani.
Kwa mujibu wa Dk. Mzindakaya, heshima kwa mwanasiasa yeyote, ni kukubali hoja nzuri za watu wengine.
“Duniani kuna vitu vitatu ambavyo vikitumiwa vizuri nchi inapata amani, mshikamano na ustawi. Pia vikitumiwa vibaya huleta vurugu na majuto. Vitu hivyo ni siasa, dini na vyombo vya habari.
Hapa tulipofikia sasa si mahali pa maandamano bali kuwaeleza wananchi ubora wa Katiba iliyopendekezwa ili wafanye uamuzi sahihi kuipitisha," alisema.

CHANZO: NIPASHE
1 comment:
Absolutely right.We do not need to see what had happened in other African countries.Kwa nini sisi kila wakati tuwe wajinga wa kukimbilia kutumia nguvu badala ya busara na utulivu?Hebu tuangalie nini walichofanya wa-SCOTLAND/UK watu wa pande mbili walikuwa na tofauti za mitazamo lakini uamuzi wa kura ulipopatikana kila upande ukawa kimya na life goes on.Sisi hapo Bongo tunataka MAANDAMANO ambayo nyuma yake kuna wabaya wenye lengo la kuleta fujo na hata kumwaga damu je TUTAFAIDIKA NINI WATU WAKIMWAGA DAMU?
Post a Comment