Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa hati ya Uraia wa Tanzania Bi.Bizimana Nyakiki Naluka mmoja wa kati ya wakimbizi 162000 kutoka Burundi waliopatiwa uraia wa Tanzania jana katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa mkoa wa Tabora jana.
Baadhi ya Wakimbizi 162000 kutoka Burundi walipatiwa uraia wa Tanzania jana mjini Tabora.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na wakimbizi 162000 kutoka Burundi waliopatiwa hati za uraia wa Tanzania katika ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Tabora jana.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Ndugu Abdulrahman Kinana akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya Rais kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma ambapo ataongoza vikao vya CCM. Wapili kushoto ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na watatu kushoto ni Makamu wa CCm Bara Ndugu Philip Mangula.
Baadhi Wanachama wa Umoja wa Vijana wa CCM mkoa wa Dodoma wakimvika skafu na kumkaribisha Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma ambapo anatarajiwa kuongoza vikao vya ngazi ya juu vya CCM.
(picha na Freddy Maro)






1 comment:
Asante kiongozi wetu mkuu. Sasa kuwatambua WaTanzania wenu walioko nje mmekataa ila mnawatambua sana wakimbizi wa Rwanda , Burundi na kadhalika. Hwa jamaa wana utajiri wa kutisha na wengine wao ni wafanyibiashara wakubwa hapa bongo!!
Post a Comment