Taarifa kutoka kwa ofisi ya Bwana Sata mwenye umri wa miaka 77 ilisema Rais amekwenda nje kwa matibabu ingawa haikusema ni katika nchi gani.
Rais Sata alijitokeza hadharani tarehe 19 Septemba kuambia bunge la taifa kuwa bado yuko hai.''Mimi sijafa'' alinukuliwa akisema Sata.
"Anajulikana kama ''King Cobra" kwa kauli zake kali, na alichaguliwa Raia wa Zambia mwaka 2011.
Haijabainika ikiwa atarejea Ijumaa kuongoza sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa nchi hiyo.
Bwana Sata hajaonekana hadharani tangu kurejea kutoka katika mkutano wa baraza la Umoja wa Mataifa mwezi jana ambako alikosa kutoa hutuba aliyotarajiwa kutoa.
Waziri wa ulinzi , Edgar Lungu, ameteuliwa kama Rais wa muda kufuatia hali mbaya ya afya inayokabili Rais Michael Sata.
BBC
2 comments:
Hii yahuzunisha kweli. Sio kila mara waskia mtu wa maana kama huyu apatikane na matatizo kama haya. Kinachinihuzunisha ama kunipa wasiwasi ni wanajeshi.
Zaidi ya as ilimwandika 90% ya waliotangaza nia ya kugombea uraisi Tanzania wako above 60 years, wakiwa katika ngwe ya 2 watakuwa ktk Sata age..
Post a Comment