Mshtuko! Siku chache baada ya kujiengua kwenye nafasi ya uenyekiti katika Klabu ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ anadaiwa kufutwa uanachama wa klabu hiyo.
Chanzo cha ndani ya klabu hiyo kimepenyeza madai kuwa, wameamua kumvua uanachama Steve kwani wanaona ni ‘kirusi’ ndani ya klabu kutokana na mwenendo wake.
“Steve amekuwa akiwashawishi baadhi ya memba wajiunge na upande wake, tofauti na umoja wa Bongo Movie Unity, viongozi wameamua kumfuta kabisa uanachama,” kilisema chanzo na kuongeza:
“Amewatangazia wenzake vibaya juzikati alivyokwenda Dodoma kwenye sherehe za kukabidhiwa kwa Rasimu ya Katiba Iliyopendekezwa kwa kuwaambia viongozi wa serikali kwamba wasanii ambao hawakwenda mjini humo ni Ukawa wakati si kweli.”
Baada ya chanzo chetu kujiridhisha na data hizo za ndani, mwanahabari wetu alimtafuta Steve Nyerere ili kujua anazungumziaje juu ya ishu hiyo ya kuenguliwa klabuni na mtazamo kuhusu suala hilo, alipopatikana alikuwa na haya ya kusema:
“Mimi ni mwanachana wa Bongo Muvi kama nimefutwa sijui lakini ni mwanachama. Kuhusu kuwasemea nilipokuwa Dodoma, ningewasemea mimi kama nani? Sina cheo cha kuwasemea wenzangu.
Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na tafrani kubwa Bongo Muvi huku madai mengi yakielekezwa kwa Steve.
No comments:
Post a Comment