ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, October 11, 2014

TUZO YA AFRICA YAMNUKIA NGASSA

Mrisho Ngassa 
Ngassa bado anaongoza kwenye orodha hiyo akiwa amefunga mabao sita katika michuano hiyo sambamba na El Hedi Belameiri wa Es Setif ya Algeria, Haythem Jouini wa Espérance de Tunis ya Tunisia na Ndombe Mubele wa As Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo lakini yeye anawazidi 
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mrisho Ngassa, anatakiwa kusali sala moja pekee ili aweze kuchukua tuzo ya Mfungaji Bora katika Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya michuano hiyo kufika fainali.


Ngassa bado anaongoza kwenye orodha hiyo akiwa amefunga mabao sita katika michuano hiyo sambamba na El Hedi Belameiri wa Es Setif ya Algeria, Haythem Jouini wa Espérance de Tunis ya Tunisia na Ndombe Mubele wa As Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo lakini yeye anawazidi kwa vigezo.


Mshambuliaji huyo wa Taifa Stars anatakiwa kusali ili washambuliaji Balameir wa Setif na Mubele wa As Vita wasifunge kwenye mechi yao ya fainali ili aweze kuchukua tuzo hiyo. Vita na Setif zitacheza fainali ya michuano hiyo Oktoba 26 na marudiano Novemba 1 mwaka huu.


Ngassa anaweza kuchukua tuzo hiyo kutokana na kufunga mabao hayo akiwa amecheza mechi nne pekee tofauti na washambuliaji wengine waliocheza mechi nyingi. Ngassa pia anabebwa na kigezo cha kufunga mabao hayo mapema tofauti na wachezaji wengine waliomfikia baada ya muda mrefu.


Mshambuliaji huyo wa Yanga alifunga mabao hayo kwenye mechi ya hatua ya awali ya michuano hiyo dhidi ya Komorozine de Comoro ya Comoro ambapo alifunga matatu ‘Hat Trick’ jijini Dar es Salaam na mengine matatu kwenye mechi ya marudiano mjini Moroni, Comoro.
Credit:Mwanaspoti

No comments: