ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, October 16, 2014

WALIMU NA WANAFUNZI WAJISAIDIA VICHAKANI .

Mh Ezekieli Maige Mbunge wa jimbo la msalala.

Na Mohab Matukio 
SHULE ya msingi Izuga Kata ya ( Isaka Jana) katika halmashauri ya Msalala wilayani Kahama Mkoani Shinyanga haina vyoo vya walimu na wanafunzi hali ambayo walimu pamoja na wanafunzi inasababisha kujisaidia vichakani kwazamu.

Hayo yalibainika katika risala iliyosomwa na afisa mtendaji wa Kijiji hicho Reuben Macheyeki mbele ya mbunge wa jimbo la Msalala Ezekiel Maige ilisema kwamba shule hiyo tangu ijengwe mwaka 2009 haijawahi kuwa na choo cha kudumu kwa walimu na wanafunzi hali ambayo inasababisha huduma hiyo kuifanyia vichakani.

Aidha risala hiyo ilisema kuwa shule hiyo yenye walimu saba na wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la sita 522, awali kulikuwa na vyoo vya muda ambavyo hata hivyo vilianguka kutokana na kunyesha kwa mvua za masika kwani havikuwa  imara.

Akizungumza na gazeti la nipashe   afisa mtendaji wa Kata ya isaka jana . Nzenze Champion alisema ni kweli shule hiyo haina vyoo vya walimu na wanafunzi, lakini mbali na uhaba huo pia shule hiyo inaupungufu wa madarasa takribani matatu kwani kwa sasa yapo manne.

Alisema walishakaa kikao cha kamati ya Shule na serikali ya Kijiji tangu mwaka jana ili kuhamasisha kuanza kwa michango ya wananchi kwaajili ya kuchimba vyoo lakini utekelezaji wake umekuwa hafifu kutokana na jamii kushindwa kuwa na mwitikio.

Hata hivyo alisema kutokana na maelekezo waliyopewa na mbunge Maige kwamba wafanye jitihada za makusudi kwa kuanzisha mchango ili kupata usaidizi kutoka kwa wadau wa elimu na wafadhili mbalimbali ambapo Maige alitoa Shilingi laki mbili ili shughuli hiyo ianze mara moja.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji hicho Mbunge huyo aliwataka viongozi wa serikali ya kijiji kukaa na kupanga mchakato wa kuanzisha ujenzi wa vyoo ili kupunguza aibu iliyopo kwa sasa katika  shule hiyo.

Maige alisema suala la ujenzi wa choo ni la wananchi hivyo halihitaji kuwa na mvutano badala yake ni kuweka ushirikiano na hatimaye kukamilisha ujezi wa vyoo vya shule hiyoo kuliko kukalia malumbano baina ya uongozi na wananchi pamoja  na kusubili serikali.

“Suala la choo ni la kwenu wananchi wa kijiji hiki, ni lazima mshiriki kikamilifu, kwanza mimi nilizani kwamba pengine tayari mmeshaonesha nguvu zenu mnahitaji usaidizi kumbe hata nguvu yenu haipo, viongozi kaeni muanzishe mchango”,alisema Maige.

No comments: