Wanafunzi 39 wa Shule ya msingi ya Fahari jijini Dar es Salaam wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Zakhem, baada ya kunywa maji yanayohisiwa kuchanganywa na mafuta ya petroli.
Hata hivyo, wanafunzi watatu wanashikiliwa na Jeshi la polisi wakituhumiwa kuhusika na tukio hilo.Tukio hilo limetokea jana asubuhi wakati wakipata chai na kunywa maji hayo yaliyohifadhiwa kwenye plastiki maalum linalomilikiwa na shule hiyo.
Mwalimu wa zamu, Ali Elias, alisema tukio hilo limesababisha wanafunzi wa madarasa yote kuathirika.Alisema shule hiyo ina utaratibu wa kuweka maji safi na salama kwenye plastiki maalum lenye koki ya kufungulia, hivyo siku ya tukio baada ya wanafunzi hao kupata mlo walitumia maji hayo kwa ajili ya kunywa.
“Walikunywa maji kama ilivyo kawaida tukiwa pale shuleni, lakini ilipopita saa mbili tulishtukia watoto wakilalamika kuumwa na tumbo, kuharisha na baadaye wailiishiwa nguvu,” alisema Elias.
Alisema katika awamu ya kwanza watoto zaidi ya 20 walikimbizwa katika hospitali hiyo na kuwa wakati wanapatiwa huduma, wanafunzi wengine waliongezeka.
Alisema katika uchunguzi wa awali walibaini kuna wanafunzi walihusika kuchanganya maji hayo na mafuta ya petroli kwa kutumia mirija ya juisi.
Muuguzi wa zamu, Silvia Sambu, alisema watoto wanane wamelazwa kwa ajili ya matibabu zaidi, huku 31 wameruhusiwa kurejea shuleni kwao baada ya hali zao kuwa nzuri.
“Tunawahudumia na hali zao zipo nzuri na wakati wowote tutawaruhusu wote,” alisema Sambu.
Kamanda wa mkoa wa kipolisi wa Temeke, Kienya Kienya, alisema analifuatilia tukio hilo kwa karibu, lakini hakuwa tayari kulizungumza kwa jana.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment