Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue naye alikuwepo katika ujumbe huo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile akifurahia jambo na Mkuu wa mambo ya uchumi wa Mfuko wa changamoto za milenia. Wakiwa pamoja na Kamishna wa Fedha za Nje Bw. Saidi Ngosha Magonya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile akifurahia jambo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue. Wakishuhudiwa na Bw. Abbas Abeid Missana Mwambata wa uhamiaji Ubalozi wa Marekani wakwanza kutoka kulia na Bw. Laston Msongole ambaye ni Mtendaji Mkuu wa mfuko wa milenia wa awamu ya pili wa mwisho kutoka kulia.
Dr. Servacius Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali wakiwa pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakiusikiliza kwa makini ujumbe wa Mfuko wa Changamoto za Milenia.
Ujumbe wa Tanzania ukiwa katika kikao cha majadiliano pamoja na uongozi wa mfuko wa changamoto za Milenia Mjini Washington Dc.Balozi wa Tanzania nchini Marekani – Washington Mhe.Liberata Mulamula pamoja na aliyekuwa Balozi wa zamani wa ubalozi huo Bw. Ombeni Sefue wote walikuwepo katika mjadala huo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile wakiwa pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Ombeni Sefue wakibadilishana mawazo kuhusu mkutano ambao ulianza muda mfupi baadae katika jengo maarufu la MCC mjini Washington DC. Marekani.

No comments:
Post a Comment