
Wachezaji wa timu ya Yanga, wakicheza kwa pamoja kumpongeza mwenzao Haruna Niyinzima baada ya kuifungia timu yake bao la pili katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania bara uliochezwa leo jioniu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam dhidi ya JKT Ruvu. Katika mchezo huo Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1, ambayo yalifungwa na Kelvin Yondani katika dakika ya 35 na Haruna Niyonzima kaika dakika ya 68, huku bao la JKT Ruvu likifungwa na Jabir Aziz katika dakika ya 90.
Mohamed Faki wa JKT Ruvu, akimiliki mpira kumdhibiti kiungo wa Yanga Haruna Niyonzima, wakati wa mchezo huo.
Beki wa Yanga anayekaribia kumsugulisha benchi Oscar Joshua, Edward Manyama (kulia) akimtoka beki wa JKT Ruvu, Madenge Ramadhan.
Jenilson Santos 'Jaja' (kulia) akichuana kuwania mpira na beki wa JKT Ruvu, Madenge Ramadhan.
Sehemu ya mashabiki wa Yanga waliojitokeza kushuhudia mchezo huo.
Mashabiki wa Yanga wakifuatilia mchezo huo.

Jaja akitafuta mbinu za kuwatoka wachezaji wa JKT Ruvu.

Jaja akichuana na beki wa JKT RUVU, Madenge Ramadhani.

Mashabiki wa Yanga wakiishangilia timu yao.

Kipa wa JKT Ruvu, Jackson Chove akiruka juu kuokoa hatari langoni mwake.

Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao lililofungwa na Kelvin Yondani katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
Jaja akitafuta mbinu za kuwatoka wachezaji wa JKT Ruvu.
Jaja akichuana na beki wa JKT RUVU, Madenge Ramadhani.
Mashabiki wa Yanga wakiishangilia timu yao.
Kipa wa JKT Ruvu, Jackson Chove akiruka juu kuokoa hatari langoni mwake.
No comments:
Post a Comment