Dada Aisha Sharrif akiendesha utaratibu mzima wa masuali na majibu kwa watoto wa kiislam, kuwajenga kiimani na dini yao, na baadae kupatiwa zawadi ya vitabu vya quran.
Mungu amlipe kila kheri na ampe moyo wenye kuendelea na imani, Amin
Wanafunzi wa dada Aisha Sharrif waliosoma quran, khadith na kutoa mawaidha, walikabidhiwa zawadi zao kutoka balozi Ali Karume, Mukhtar ni mmoja wa wanafunzi hao pia akiwa MC katika program yao, akipewa zawadi yake kutoka kwa balozi Karume
Zuhura (Ulah) akiwa na mwalimu wake dada Aisha Sharrif kushoto, akisoma khadith mbele ya waumin wa kiislam katika sherehe hiyo ya Eid Maryland, USA
Dada Aisha Sharrif, muandaaji wa program na zawadi za watoto, wote walipata zawadi, aliejibu masuali na wale walibakia bila kuulizwa masuali pia walipata zawadi na wao. dada Aisha anawaomba wazazi kuhakikisha watoto wote waliopata zawadi wazifanyie kazi, ni zawadi nzuri kwao
Mtoto Sarah akisoma suratul ikhlas na kitafsi mbele ya mwalimu/mama yake ambae ni muandaaji wa program hiyo ya watoto siku ya Eid, Sarah kwa utulivu alisoma mwanzo hadi mwisho na tafsiri yake bila kutetereka, "TAKBEER"JUU NA CHINI
Elias kulia akisoma suratul Arrahman, kushoto Mukhtar akifanya tafsiri kupitia kwenye simu
No comments:
Post a Comment