ANGALIA LIVE NEWS

Monday, November 24, 2014

Chadema waichana Serikali kuhusu maabara

Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje

Mwanza. Wabunge wa Kenya kupitia Chama cha ODM wameeleza kushangazwa kwao kwa kuona Watanzania wanachangia fedha kwa ajili ya kununua madawati, wakati nchini yao ina maliasili nyingi walizosema zingetosha kufanya maendeleo bila wao kuchangishwa.
Wakihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika sanjari na harambee ya kuchangia wajasiriamali, kwenye Viwanja vya Mbugani mkoani hapa jana, wabunge hao Nicolous Gumbo na Peter Kamu walisema kuwa hata Wakenya wanaitamani Tanzania kwa jinsi ilivyo na vivutio vingi.
Walisema kuwa Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya, Raila Odinga anapenda watu wanaowajali wananchi, huku wakitolea mfano kama anavyofanya mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje kwa kuwakumbuka wananchi na kutaka kuwainua kiuchumi.
“Kwa kweli Tanzania ni nchi nzuri imezungukwa na maliasili nyingi mfano kuna Ziwa Victoria, lakini leo inashangaza kuona kila kona kunakuwa na michango mfano tatizo la madawati, wananchi wanachangishwa fedha,” Kamu.
Aliongeza: “Matatizo kama haya yangeweza kumalizika kwa kufanya uamuzi sahihi wa kusimamisha watu wa kina Wenje, Msigwa kwani wanaweza kufanya mabadiliko makubwa.”
Naye Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa (Chadema) alisema kuwa jambo la msingi linapaswa kufanywa na Watanzania ilikuwa na maendeleo ni kufanya mabadiliko ya uongozi na kujituma kwenye shughuli zao za kila siku ili kujikwamua kiuchumi.
Mbunge mwingine kutoka Kenya Nicolous Gumbo, alisema kuwa ni vyema kwa viongozi kuwakumbuka wananchi ambao wamekuweka madarakani na siyo kufanya tofauti kama vilivyo vyama vingine.
“Kuna watu wakipata nafasi za uongozi kamwe hawezi kuwakumbuka wananchi wao wanasubiri hadi kipindi cha uchaguzi ndio wanarudi tena. Wananchi wa Mwanza nawaomba msikubali kufanyiwa hivyo kama mtu hawajali, achaneni naye,” alisema Gumbo.
Mbunge wa Nyamagana ambaye ndiye aliyeandaa harambee hiyo, Ezekiah Wenje alisema kuwa ameguswa kufanya hivyo ili kuwainua wananchi wa jimbo lake, hasa watu wenye kipato cha chini.
“Nimegushwa kufanya hizi, kwani lengo langu ni kutaka kuona wananchi wenye kipato cha chini maisha yao yanainuka. Tutaweza kuwasaidia kwa kuwapa fedha za kuanzisha mitaji ili kuweza kujikwamua kiuchumi kwa kujiajiri wenyewe,” alisema Wenje ambaye alichangia Sh7 milioni.
Chadema hicho pia kipo katika operesheni ‘Delete CCM’ inayoendelea nchi nzima ambapo viongozi wake wanazunguka mikoa mbalimbali kuendesha kampeni ya kuking’oa madarakani chama tawala, CCM.
MWANANCHI

No comments: