Ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Costa lenye namba za usajili T 336 CJY ambalo lilipinduka baada ya kumshinda dereva wakati akijaribu kulikwepa gari linguine aina ya Suzuki lenye namba za usajili T 327 ARZ.
Kwa mujibu wa baadhi ya majeruhi walionusurika kwenye ajali hiyo walisema chanzo ni dereva kushindwa kulimudu gari la abiria baada ya kulikwepa gari dogo kutokana na kuwa na mwendokasi pamoja na mvua kubwa iliyokuwa ikiendelea kunyesha.
Baadhi ya majeruhi walikimbizwa katika Hospitali teule ya Ifisi na wengine wakipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajili ya matibabu zaidi.
Baadhi ya majeruhi wakitafuta mizigo yao mara baada ya kutoka ndani ya basi hilo
Baadhi ya abilia wakitaka kumpiga Dereva wagari ya aina ya Suzuki kuwa yeye ndio alisababisha ajali hiyo kwa kuyumbayumba kwake barabarani
Moja ya wasamaria wema akiwazuia abiria wenye hasira kali kutaka kumpiga mzee huyo Mwenye Suzuki ambae alijulikana kwa jina moja tu mzee Mtawa
Mwandishi wa habari Kenneth Mwazembeakiwasili katika Hospitali ya Ifisi akisindikizwa na Joseph Mwaisango wa Mbeya yetu baada ya kupata ajali eneo la Senjele wilayani Mbozi akiwa anatokea shambani kwake huko wilayani Momba kwa taarifa za awali inasemekana amevunjika mguu wa kushoto
Picha na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment