Ni siku nyingine ya Jumanne ambapo tunakutana katika safu yetu hii mahususi kwa kuelimishana na kukosoana kwa lengo la kuboresha uhusiano wa kimapenzi na wenza wetu.
Baada ya wiki iliyopita kuzungumza nanyi kuhusu madhara ya kuchunguza simu ya mume, leo nataka kuzungumzia ‘topiki’ kuhusiana na wanawake wanaopenda kutoa siri za wapenzi au waume zao nje.
Nimeamua kuzungumzia ishu hiyo kwa sababu nimeshuhudia mara kadhaa wanawake wakiachwa, kisa kikiwa kuwaeleza wenzao mambo yao ya ndani.
Tabia hiyo imeshamiri sana siku hizi ambapo wanawake hutoa siri za waume zao wakifikiri watasifiwa na wenzao kumbe wanajiharibia.Utamsikia mwanamke aliye kwenye ndoa akiwaambia wenzake jinsi mumewe alivyo goigoi wakati wa makesheshe jambo litakalowafanya wenzake kumbeza mumewe kwamba ni mwanaume suruali nk.
“Jamani mnamuona mume wa Khadija alivyopendeza? Lakini huwezi amini kwenye yale mambo yetu hawezi kitu,” mmoja wa shoga zako atawaambia rafiki zake baada ya kumuona mumeo akirejea kutoka kazini, chanzo ni wewe kutoa siri hiyo nje.
Wengine, ili waonekane wameolewa na wanaume waliojaaliwa utundu na mambo mengi ‘uwanjani’, huwasifia kwa wenzao namna wanavyofurahia mapenzi pasipo kujua kama wanawapa mwanya wa kuwaibia penzi lao.
Utamsikia mwanamke ambaye mumewe ni mtu wa dili akiwaambia wenzake kwamba mumewe kaporomosha bonge la mjengo huko Mbezi Beach, kanunua Coaster au benzi mbili na kufungua miradi kibao.
Hivi shoga yangu unafikiri mumeo akijua unavyovujisha siri zake atakuacha, ni wazi atakupiga chini kwa sababu atabaini unaweza kusababisha aanze kuchunguzwa anakozipata fedha kisha kukamatwa na kuishia gerezani.
Shoga yangu, mwanamke unatakiwa kuwa msiri wa mambo yote unayofanya na mumeo hata kama jamaa ana tatizo la kukojoa kitandani mfichie siri hiyo.Hebu fikiria siku akigundua siri kuhusiana na tatizo lake la kukojoa kitandani au kukoroma kama mlevi wa gongo akilala usiku umewaambia wenzako, patakalika kweli?
Naamini hakuna mwanaume anayeweza kuvumilia upuuzi huo, ni wazi atakutimua na nafasi yako itachukuliwa na mwenzako anayejua kutunza siri za ndani.
Tuonane wiki ijayo kwa mada nyingine.
GPL
1 comment:
inasikitisha na inashangaza at the same time inafurahisha tena nakupa cheko lako mwandishi wa habari hii haaaaaaaaaaaaaaaaaa haaaahaa.
unavyosema ni kweli kutolea siri za ndani za mumeo si vizuri lakini hujui siku hizi wanaume nao pia wanawatolea wake zao siri za ndani wakati"KUCHAPIA SIRI ZA NDANI".
Mnawasema sana wanawake kila leo kama mnawafunda hivi sivyo.wanaume nao wanahitaji kufundwa maana siku hizi wao wamekuwa wambea kuliko hata wanawake si siri chunguzeni mtaona.
na jambo la kuchekesha ni hivi "KWANI UKIACHWA HAKUNA WANAUME WENGINEWE MBONA WAMEJAA TELA MITAANA KILA PEMBE.NA SIKU HIIZI WANAUME NAOWANATAFUTA KUSTIRIWE KUWA KINA "MARIO"NA WANATAFUTA WAKE.
AKIKUACHA RISKI YAKO IMEKWISHA KWAKE UTAPATA MWINGINE KWANI ALIKUPATAJE WEWE MWINGINE USHINDWE KUMPATA.
mwanamke mwenye ujasiri na mwenye heshma atatulia kwa mume,mume akimletea zake za kuleta atasepa na atapata mwinginewe............
usawa usawa haki sawa kwa woteeeeeeeeeeeeeeeeeeee.
unachwa leo kesho anakuja mwingineweeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.
bembeleza nikubembeleze hunibembelezi sikubembelezi."HUWEZI KUNICHAPIA VIZURI NDANI"Nitatafuta mwinginewe anayeimudu kazi na tutalaaaaa kwa raha zetu.............
Post a Comment