Advertisements

Friday, November 14, 2014

DIAMOND, ZARI GUMZO AIRPORT

Zari au The Boss Lady akimwelekeza kitu mpambe wa 'Diomond'. aliyejulikana kwa jina la Q Boy pamoja na kwamba Diamond alikuwemo kwenye gari hilo siti ya nyuma hakushuka Airport kila kitu alimwachia mpambe wake afanye ikiwemo kumsindikiza Zari ndani ya uwanja wa ndege.

Musa Mateja na Imelda Mtema wa GPL

BAADA ya kula bata za kutosha Bongo, wakati wakisindikizana kimahaba, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mrembo mkali kutoka Uganda, Zarinah Hassan a.k.a Zari au The Boss Lady, wamezua gumzo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar, Ijumaa lina mchapo kamili.

HABARI KAMILI
Tukio hilo lililoshuhudiwa na wanahabari wetu lilijiri mishale ya mchana, Jumanne iliyopita katika maegesho ya airport (uwanja wa ndege) ambapo Diamond alikuwa akimsindikiza Zari aliyekuwa akitimua Bongo baada ya kufanya yao kwa siku kadhaa.

KABLA YA TUKIO
Awali kabla ya tukio hilo, gazeti hili lilipokea ‘ubuyu’ kutoka kwa chanzo chake cha kuaminika kwamba, wawili hao walikuwa wakijiandaa katika hoteli waliyokuwa kwa siku kadhaa iliyopo kwenye Ufukwe wa Bahari ya Hindi, tayari kuelekea uwanja wa ndege.

“Ijumaa acheni kulaza damu, kwa taarifa yenu Diamond ndiyo anajiandaa kumpeleka Zari airport wahini pale mpate tukio kamili ili kumaliza ubishi kuwa kweli walikuwa wote Bongo,” kilisema chanzo hicho kikiomba hifadhi ya jina gazetini.

IJUMAA MZIGONI
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, wanahabari wetu walitia gia kwenye ‘motokaa’ ambapo dakika kadhaa baadaye walikuwa wametega satelaiti zao uwanjani hapo tayari kwa kunasa tukio.

BMW X6 LATOKEA
Wakati wanahabari wetu wakiwa wanakaribia kukata tamaa, ghafla lilitokea gari jeusi aina ya BMW X6 ambalo tofauti na magari mengine, badala ya namba za usajili, lenyewe lilikuwa na maandishi yaliyosomeka kwa herufi kubwa ‘PLATNUMZ’ kisha likapaki kwenye eneo la maegesho uwanjani hapo.
Gari hilo lilikuwa likiendeshwa na kijana mmoja wa Diamond aliyejulikana kwa jina la Q-Boy na pembeni mwake kwenye siti ya abiria alikuwepo mpambe mwingine wa msanii huyo ambaye jina halikupatikana.

DIAMOND AJIFUNGIA
Wakiwa siti ya nyuma, wakati Zari anashuka, Diamond alijifungia kwenye gari ili kuwakwepa mapaparazi baada ya kuwashtukia kuwa walikuwa wakimsubiri.

WAZUA GUMZO
Wawili hao walizua gumzo uwanjani hapo ambapo baadhi ya watu wakiwemo Wazungu walikuwa wakiwashangaa huku Wabongo wakitamani Diamond atoke kwenye gari amtambulishe Zari kama ndiye mrithi wa Wema au la!

“Huyu Diamond naye balaa. Kampata wapi mtoto mrembo kiasi hiki? Hakyanani na mimi bora niwe msanii nitafaidi. Mtoto kaumbika hasa,” alisikika mmoja wa madereva teksi huku wenzake wakimkatisha tamaa kuwa hawezi kuwa msanii. Zari alishuka na yule mpambe wa Diamond na kuambatana hadi sehemu ya kukaguliwa ili akapande ndege.

IJUMAA LAMBANA ZARI
Kabla ya kufikia sehemu hiyo, wanahabari wetu walibahatika kumfotoa picha za kutosha Zari kisha kumfuata na kumuuliza alikuwa na ishu gani na Diamond ambaye alikuwa naye hotelini Bongo kwa takriban siku tano.

Hata hivyo, Zari alishindwa kujibu na kuishia kusema kuwa hana maoni.“No comment,” alisema Zari na hata alipoombwa kufafanuzi kidogo aligoma.

DIAMOND AFUNGUKA
Baada ya tukio hilo, wanahabari wetu walimtafuta Diamond kwa njia ya simu ili azungumzie kwa kina juu ya uwepo wa Zari Bongo na tuhuma za kujihusisha naye kwenye mapenzi ambapo Diamond alifunguka:

“Niliwaona airport mkimpiga picha na gari langu na mkaongea naye.
“Kweli ninyi ni noma sana, lakini nadhani mliandika hivi karibuni kuwa mimi nimeachwa na Wema (Sepetu).

“Ukweli hakuna mwanaume anayeweza kujitoa kwa demu wake hasa kumpatia zawadi ya gari kama niliyotoa kwenye bethidei ya Wema halafu baadaye usikie kuna mwanaume mwingine katoa zaidi na ukaendelea kufurahia.

ZARI NI RAFIKI TU JAMANI!
“Sitaki kuongea mengi ila Zari naomba atambulike kama rafiki yangu tu jamani.”

YATOKANAYO
Hivi karibuni Diamond alimwagana na Wema ambapo siku chache baadaye habari zilivuja kwamba Zari ambaye ni msanii wa kike tajiri Afrika Mashariki ndiye mwenye uwezo wa kuziba pengo hilo mara tu baada kuonekana na jamaa huyo.

No comments: