Wagombea nafasi ya Mwenyekiti Jumuiya ya Watanzania Seattle jimbo la Washington Emil Mutta na Fatma Tamim wakijinadi na kujibu maswali mbalimbali kutoka kwa wapiga kura wao siku ya Jumapili Novemba 2, 2014 siku ulipofanyika uchaguzi wa Mwenyekiti na Emil Mutta kushinda kwa asilimia 72 kwa wapiga kura 184 waliojitokeza kati ya jumla ya Watanzania waishio jimbo hilo wanaokadiriwa kufikia 600.
Joshua Gwakisa(aliyesimama) akiuliza swali kwa Wagombea wenyekiti (hawapo pichani) siku ya uchaguzi Jumampili Novemba 2, 2014 Seattle jimbo la Washington na Emil Mutta aliibuka mshindi wa kiti hicho kwa temu ya pili mfululizo baada ya ile ya kwanza ya miaka 2 kumalizika.
Emil Mutta akipiga kura nafasi ya kumtafuta mwenyekiti baada ya ule uchaguzi wa viongozi wa jumla nafasi ya mweyekiti uchaguzi ulivurugika na ndio maana ukapelekea kurudiwa kwa nafasi ya mwenyekiti ambayo waliokua wakigombea ni Emil Mutta ambaye ndiye aliyekua Mwenyekiti kwa uongozi uliopita huku Fatma Tamim akiwa katibu wake,
Fatma Tamim ambaye kwenye uongozi uliopita alikua katibu nae akipiga kura nafasi ya mwenyekiti ambaye nae alikua akiigombea kwenye uchaguzi uliofanyika siku ya Jumapili Novemba 2, 2014 jijini Seattle jimbo la Washington.
Bi. Aziza ambaye yupo kwenye kamati ya uchaguzi akihakiki wapiga kura wake.
Bwn. Salmin akitumia haki yake kumchagua mwenyekiti.
Bi. Aziza (kushoto) akimhakiki Dullah na mama mwenye nyumba wake siku ya Jumapili Novemba 2, 2014 siku ulipofanyika uchaguzi wa mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania jimbo la Washington (sio Washington, DC)
Mayor wa Seattle Amin Dolla akipiga kura yake.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
Bwn. Filfil akijiandikisha tayari nae kupiga kura
Mjumbe bi Asha akijiandikisha tayari kwa kupiga kura kwenye uchaguzi wa mweyekiti uliofanyika siku ya Jumapili Seattle jimbo la Washington.
Bwn. Edward Ngayoma mmoja wa wanakamati ya uchaguzi akimhakiki mpiga kura wake.

Watanzania wa Seattle, Washington State wakisubili zamu yao ya kupiga kura.
Watanzania wa Washinton State wakisubili kupiga kura huku wengine wakiwa na shauku ya kumjua mshindi wa nafasi ya uenyekiti.
Bwn. Dullah (kulia) akionyesha namba yake aliyopigia kura.
Watanzania wa Washington State wakiwa kwenye mstari wakisubili kuandika historia.
Mtanzania wa Washington Seattle akitumia haki yake ya msingi.
Bwn. Joshua Kwakisa akipiga kura.
Mdau Ubwa nae akipiga kura.
Kupiga kura kukiendelea.
Bwn. Haroub Kenwood akitumia haki yake ya msingi kupiga kura kwenye uchaguzi wa mwenyekiti jimbo la Washington.
Bi. Samia Mshangama akiendelea na zoezi la upigaji kura.
Mdau Jimmy Mkude akitumia haki yake ya msingi katika uchaguzi wa Mwenyekiti uliofanyika siku ya Jumapili Novemba 2, 2014 jimbo la Washington.
Toka kushoto ni Bi.Lilia Mutta, Emil Mutta, Eddie, Ameir Jecha na Bi. Ellie Cooper ambaye ni dada ya Lilian mke wa Emil Mutta ambaye yeye anaishi DMV.






















3 comments:
Samahani lakini tunaomba muandike taarifa za ukweli kuhusu uchaguzi wa Seattle.
Kura hazikua 184 ila kura zilikuwa 84.
Bi.. Fatma alipata kura 35 ambayo ni asilimia 41.6% na Bw. Muta alipata kura 49 ambayo ni asilimia 58.3%
Tunaomba tuhakikishe taarifa kabla ya kuziweka uwanjani.
Asante,
Mpiga kura na mdau mkazi wa jimbo la Seattle,WA
Tunaomba muwe mnaweka comment za watu wanazotoa bila kuchagua. Sheria ya hapa USA ni freedom of speech. Jana niliandika comment kuhusu uchaguzi haijawekwa na kuna wakati iliandikwa comment ya kukusoa taarifa pia haijawekwa. Kwa hiyo sasa itabidi tutangazie kuwa vijimambo huchagua comment kwenye mablog mengine. Hii sio personal attack kwa vijimambo bali tunataka tupewe habari za ukweli.
Madu Msema Ukweli
nataka kuliza tu hivi wanafanya mambo haya ya kuchagua jumuiya za kila state ili iweje au kwa manufaa ya nani?wabongo mlio huko majuu kweli mna vijimmambo si vidogo haaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.
Post a Comment