"Hatukubali! ...fedha kuibwa halafu wezi wanaishia kujiuzulu tu"
Lazima bunge lichukue uamuzi mgumu. Lazima waziri mkuu apumzike, Baraza la mawaziri livunjwe, serikali iundwe upya na isimamie jukumu la kuwapeleka mahakamani raia na viongozi wote waliohusika ama kufanikisha au kupokea mgao wa fedha za ESCROW.
Na kisha pamoja na kuwashtaki, lazima hasa warejeshe fedha hizo, kisha wakapumzike kwenye magereza zetu bora.PERIOD!
Supu ya mbwa hunywewa ikiwa ya moto
Ujumbe huu umeandikwa na Julius Mtatiro kupitia mtandao wa fb na Vijimambo imeupata kupitia Wavuti Blog
17 comments:
TUMECHOKA
NASAPOTI KWA ASILIMIA MIA MOJA. Huu ni uhuni haiwezekaniki kila leo utasikia fedha zimeliwa , fedha zimegawiwa na wahusika kuhamishwa idara bila kuchukuliwa hatua kwanini!?? Raisi unafanya nini? Waziri mhusika na kitengo cha fedha uko wapi? Wakati umefika hakuna kuchekeana wala kuoneana huruma hizi ni fedha za walipa kodi. JIUZULUNI KAMA HAMUWEZI KUFANYA KAZI IPASAVYO. Fuateni utaratibu kama nchi nyinginezo zinavyofanya mfano Amerika kosa hata likifanywa na wa chini aliyeko juu anajiuzulu. Tusidanganyane.
hakuna wazalendo wa kweli Tanzania na Africa izima zaidi ya hayati nelson mandela alipigania nchi yake na watu wake.
hii salala la escro litazimwa tu kiusanii.mtu akirambishwa asali basi kwisha kazi.
ndo serikali ya mafisadi ilivyoo.
peleka motto wako na wewe shule unajifunza na kujifaa katika maisha yako mambo haya unawachia wenyewe mafisadi.mwisho wa siku mungu anawaona na atawahukumu. AMEN
kama haka kaujumbe kamekugusa unafanyaje aumeamuaje? mbona wewe ndo wakwanza kuziziba comment zinazowasema magamba wenzako na ufisadi wao kama kweli haka kaujumbe kamekugusa.mmmwaaafyoooooooooo.
hata ikithibitika Fedha za Escrow ni za Wizi, Nawahakikishia Hakuna Yoyote wa Kuwajibika.mambo yatakwenda na kuzimika kimya kimya kutachakachuliwa,si tunasikia sasa wamenyofoa page za zile ripoti na watachakachua tu kama walivyofanya kwa katiba.thelusi haijatimia ikatimizwa.
ndo serikali yetu hii ya Tanzania.uchakachuaji kwenda mbele
Wezi ni wezi tu!. Lakini dhambi hiyo itawatafunatu. mungu anawaona na si wakuchezea mungu hapendi watu wezi na mafisadi malipo hapa hapa duniani kesho akhera hisabu tuu.
ukoo wa panga daima utakuwa uko wa panya hatoweza kuwa ukoa wa sisimizi/mdudu chungu
Wezi ni wezi tu!. Lakini dhambi hiyo itawatafunatu. mungu anawaona na si wakuchezea mungu hapendi watu wezi na mafisadi malipo hapa hapa duniani kesho akhera hisabu tuu.
ukoo wa panga daima utakuwa uko wa panya hatoweza kuwa ukoa wa sisimizi/mdudu chungu
Sisi Waafrika ni mtakataka sana na tutaendelea kuwa Masikini mpaka mwisho wa Dunia hii, hizi kelele zote ni kwa sababu tu humo ndani kuna fedha ya Mzungu, hata EPA ilikuwa hivyo hivyo wanapiga kelele kwa maana Mzungu anataka fedha yake, lkn Madini yetu yanaibiwa kila siku, Gesi yetu inachotwa juu kwa juu huko baharini, Huko Same nasikiaMadini ya Bauxite kwa wasio jua ndiyo yanayotumiwa kutengezewa Aluminium yanachimbwa na kuuzwa nje ya Nchi Mkuu wa Wilaya anajua hilo, Mkuu wa Polisi anajua hilo, Mbunge wa huko analijua hilo kwa Kifupi Serikali inajua lkn kimya, kesho wazungu wakiliongelea Utasikia UKAWA wanaanza kulivalia njuga...
Mbona Serikali wamegoma kutoa mikataba ya Madini na gesi na hakuna Mwamko wowote juu ya hilo? Kwa maana kama ni fedha, fedha inayochotwa na Wazunzu/wahindi kutoka kwenye Madini na gesi haya mambo ya sijui EPA, escrow ni cha mtoto!
tuwekeze nguvu zote kwenye Madini yetu na SIYO sijui EPA au escrow!
tunataka uwajibikaji na si maneno na kiburi cha PESA ZETU, wanachomekea suruali nzuri, wanakula vizuri,wanaheshimika kwenye familia zao na wake zao kama waume/wake bora kumbe ni pesa za wizi na si za jasho lao,wakati MTANZANIA wa kawaida akinyanyasika kulipa kodi kila bidhaa anayonunua na tayari wameshaanza mpango hadi barabara tulipie NASEMA wamezidi hapana wawajibike na kurudisha pesa zetu.Jaribu kufikiri kidogo tu mwalimu ama mtumishi wa umma analipwa kiasi gani na kwa nini analipwa hivyo wakiambiwa wapandishe walau kima cha chini kifike 315,000/= ni wakali kama MBOGO aliyejeruhiwa na risasi kumbe pesa zipo na wanakula wenye AKILI WACHACHE na Watanzania akitaabika
Ukweli ni kuwa fedha za escrow sio big deal kihivyo!, kumeishatokea maskandali makubwa zaidi ya uchotaji fedha BOT, escrow ni cha mtoto, na hakuna chochote kilichofanyika!, mfano TanGold, Deep Green, Meremeta, Import Support, DCP, etc, etc, wahusika walifanywa nini?!.
sema ni kwa sababu pesa za mzungu na mzungu anataka pesa zake ndo maana unaona watu wanafoka foka na kutoa mapovuu na kupandisha mizuka ya msukuleee.
Niliyoyasema, yameanza kutokea!, na hata ningekuwa mimi sikubali hata kido!, kwenye EPA, mijitu imeiba bilioni 40!, haijafanywa chochote!, leo watu wamemegewa tujisenti twa bilioni 1.6, alafu wabunge wanapiga kelele wahusika wawajibike!, wawajibike kwa lipi?!, angalieni Prof. Muhongo anavyo komaa!.
Umeishajiuliza kwa nini orodha ya mafisadi wa ESCROW imejaa wakiristo, nyie ndiyo mnaitafuna hii nchi kwa sababu hamjapigania na kumwaga damu zenu kwa kuupatia uhuru.hamna uzalendo wakweli.
lolote linaweza kutokea kwanza hizi pesa zimechukuliwa na wasomi wa Kikiristo Div One za Kanisa, na benki iliyotumiwa kufanyiwa mgao ni benki ya Kanisa Mkombozi na kuna Maskofu wamepokea hizo pesa unategemea nini hapo sisi wauza kahawa tupo pembeni vibarazani kwetu tunacheza bao
vijimambo team na dj usinibaniyie comment hii tafadhali lazima ukweli watu wajuweee.naja ni blog yenu
hata ningekuwa mimi sikubali hata kidogo!, kwenye EPA, mijitu imeiba bilioni 40!, haijafanywa chochote!, leo watu wamemegewa tujisenti twa bilioni 1.6, alafu wabunge wanapiga kelele wahusika wawajibike!, wawajibike kwa lipi?!, angalieni Prof. Muhongo anavyo komaa!.
Katika kikao cha ndani ya CCM, Waziri wa nishati Sospeter Muhongo amesema bayana kwamba hatishwi na wabaishwaji na kamwe hawezi kujiuzulu kutokana na chuki za mafisadi wanapigania vitalu vya gesi na kama atalazimika kujiuzulu siyo tu bunge litayumba, bali ardhi ya Tanzania itatikisika, kwa sababu anazo data za uhakika kuonyesha hili swala la IPTL ni mpango uliosukwa na madalali walionyimwa vitalu vya gesi na wale walivuliwa uwakilishi wa tanesco kisheria
akifungwa au kufilisiwa mtu kutokana na kashfa hii, naahidi kunya boga hadharani.
Hizi scandal za sijui escrow, epa, Richmond etc etc huwa hazinishitui hata kidogo. Tumezoea kuibiwa na tumezoea kuiba. Mtanzania gani sio mwizi?
Kila mbuzi anakula Kwa urefu Kwa kamba yake. Wote tunaiba Kwa nafasi tulizonazo, wizi ni mindset ya kila mtanzania as if Mungu badala ya kusema nendeni mkajaze dunia waTz alituambia "nendeni mkaibiane Tanzania"
Hatua hazijawahi chukuliwa na hazitakuja chukuliwa na wizi utaendelea nchini hata ukamilifu wa dahari. Wananchi kuweni wapole tu au ibeni Kwa nafasi zenu pia- it's that simple.
Taifa la wala rushwa...watu wanaiba benki kuu...wanatuhonga tunawachagua...halafu tunatarajia matokeo chanya kwayo.....
Tunavuna wizi tumepanda wizi...tusishangae tubadilike
Na bado tunapigia chapuo wezi wengine kushika hatamu ...kisa ameiba katosheka hatoiba tena....
Mhh kweli rushwa sabuni ya roho kwa wadanganyika
Watanzani karibia wote ni wezi ndo maana wananyamaza wakijua nao siku yao ya kuiba itafika
Post a Comment