Advertisements

Thursday, November 20, 2014

LORI LALIPUKA ENEO LA MIKUMI MKOANI MOROGORO

Tumepokea picha ya tukio la ajali ya Lori lililokuwa limebeba mapipa ya lami ambalo limeshika moto mapema leo asubuhi maeneo ya Mikumi, Morogoro.chanzo cha mlipuko huo bado hakijafahamika mpaka sasa na bado hatujapata taarifa kama kuna aliepoteza maisha au kupatwa kwa majeruhi.Chini ni ujumbe kutoka kwa mdau wetu alietuletea taswira hizi kuhusiana na hali ya barabara hiyo.
''Kama una safari ya kwenda Iringa-Mbeya au kama unapokwenda utapita mikumi basi sitisha safari kwani njia inefungwa tangu saa mbili asubuhi. Kuna lory linawaka moto mpaka sasa. Lilikuwa limebeba lami so lami bado inawaka na inesambaa sehemu kubwa''
Baadhi ya watu wakishudia tukio hilo la ajali. Picha kwa hisani ya Michuzi Media Group

No comments: