ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, November 20, 2014

WABUNGE WACHARUKA KASHFA AKAUNTI YA TEGETA-ESCROW NI SHEEEEDA

Naibu spika wa bunge Job Dungai, yeye ndiye kashikilia rungu, Ripoti " ijadiliwe au la"
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya bunge ya hesabu za serikali, (PAC), Zitto Kabwe. Taarifa ya CAG kuhusu akaunti nya Tegeta Escrow, iko mikononi mwake
Mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani bungeni, Tundu Lissu, (CHADEMA),akizunghumza bungeni mjini Dodoma jana, wakati lile sakata la IPTL, linalogubigwa na akauti iliyojichukulia umaarufu TEGETA ESCROW, lilipoibuka bungen i wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa waziri mkuu. Wabunge wanataka "ngoma" ijadiliwe bungeni, licha ya kashfa hiyo kuwa tayari mahakama kuu ya Tanzania
Mbunge wa Kigoma Kusini, (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, huyu ndiye aliyeibua kashfa ya akaunti ya Tegeta-Escrow
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na mbunge wa Urambo, (CCM), Samwel Sitta
Mbunge wa Iringa mjini, (CHADEMA), Mchungaji Peter Msigwa
Mbunge wa kuteuliwa na Rais, ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-M,ageuzi, James Mbatia
Mbunge kijana, Esther Bulaya, (CCM)
Mbunge wa Longido,(CCM), Lekule Laizer,
Mbunge wa Kasulu mjini (NCCR-Mageuzi), Moses Machali, ndiye aliyemchokoza Waziri mkuu kuhusu ripoti hiyo kujadiliwa bungeni
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, "Punguzeni jazba", akiwasihi wabunge kuwa serikali iko makini na inasubiri kwa hamu taarifa hiyo ili kila mtu hata yeye akibainika abebe msalaba wake, lakini akatahadharisha kuhusu umuhimu wa kuheshimu mihimili ya dola ikiwemo mahakama
Mbunge wa Kahama (CCM), James Lembeli Picha kwa hisani ya K-VIS Production

6 comments:

Anonymous said...

Tuweni wakweli ndugu waheshimiwa kwa manufaa ya waTanzania kwa ujumla na isiwe swala la KISIASA. Tunaomba siasa iwekwe pembeni tuangalie maisha ya waTanzania walio wengi na tuache kuangalia ya siasa tuuu!.

Anonymous said...

hakuna mtu anaye jail maslahi ya watanzania wanachojali ni matumbo yao na family zao.wizi huu kama hawajaiba wao ni nani ni mazimwi.na bado mnawabebe nakuwapigia makofi.
kama si wewe wa kuitetea nchi yako ni nani kama si leo ni lini.hakuna mkuu yeyote atakaye kutetea wewe raia wa chini.

nyinyi fokeni fokeni na kutoa mapovu ovyoooooooooooooooo kama wehuuu.

pesa zimeshachuliwa na wajanja wa hii nchii


vijimambo team msiweka hii comment tunakujuweni kwa kufagilia kwa sana mlivyoo.

Anonymous said...

kinachofanyika hapa na tukiunganisha DOT's kauli ya Zitto hapa ndani ya bunge kauli ambayo ilionekana kukubaliwa na Werema kwa ishara ya kichwa ni dhahiri CAG, PAC,CCM na vyombo vya usalama vya nchi vinataka kutupotosha wananchi na sakata hili ili waendelee kulinda hayo mafisadi na hasa kuilinda Ikulu na Pinda ambao kwa sakata hili wanawajibika moja kwa moja.

Anonymous said...

Original itakuwa ipo CAG. Sasa kama hizo pesa hazikuibiwa na ccm, ziliibiwa na mizuka? Kicks of a dieing horse!!

Anonymous said...

Kweri pesa shikamoo! ukiwa na hela nchi hii wawezafanya lolote, wamekwiba pesa na sasa wanazitumia kujilinda. Wakifanikiwa, watazitumia kujisafisha. Kweri pesa shikamoo!

Anonymous said...

hata ikithibitika Fedha za Escrow ni za Wizi, Nawahakikishia Hakuna Yoyote wa Kuwajibika.watafanya kama walivyofanya uchakachuaji wa katiba,thelusi hajatimia ikatimizwaa.ndo Tanzania