Advertisements

Thursday, November 20, 2014

MAALIM SEIF ATEMBELEA ENEO LA JENGO LILILOANGUKA JANA MJI MKONGWE ZANZIBAR

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akimsikiliza Kamanda Ame Ali ambaye ni kiongozi wa shughuli za usafishaji wa eneo lilipoanguka jengo la ghorofa huko Shangani mjini Zanzibar.
 
Na Khamis Haji , OMKR

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amezitaka Mamlaka zinazosimamia majengo katika enelo la Mji Mkongwe Zanzibar kuwa na utaratibu mzuri wa kuyakagua ili kuhakikisha uimara wake na kuepusha maafa kwa watumiaji na jamii nzima.

Maalim Seif amesema hayo wakati alipofanya ziara ya kukagua shughuli za uondoaji kifusi katika jengo lililoanguka jana katika eneo la Shangani mjini Zanzibar, zoezi linalofanywa na askari wa Kikosi cha Zimamoto, Manispaa pamoja na wananchi wa Mji Mkongwe.

Makamu wa Kwanza wa Rais amesema nyumba zilizopo katika Mji Mkongwe zinasimamiwa na Wizara ya Ardhi, Mamlaka ya Mji Mkongwe au Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana, hivyo taasisi hizo ni jukumu lao kuzigagua uimara wake na kuhakikisha ni madhuti.

Amesema pale ambapo taasisi hizo zitabaini kuna nyumba ambazo zimechakaa zinazoweza kuanguka na kuhatarisha maisha ya watu na mali zao ni vyema kuwataka watumiaji wake wahame, ili kuepusha kuangukiwa na nyumba hizo na kuhatarisha maisha yao.
Katika ziara hiyo, ambapo alifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Abdalla Mwinyi Khamis na Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe, Mhe. Ismail Jusa Ladhu alivipongeza vikosi vinavyoendesha shughuli za Uokoaji na wananchi wa Mji Mkongwe kwa kazi kubwa ya uokozi wanayoifanya.

Naye Mkuu wa Kituo cha Zimamoto na Uokozi Makao Makuu, Ame Ali ambaye anaongoza shughuli za uokozi na usafishaji wa eneo hilo amesema kazi hiyo inaendelea vizuri na walitarajia kuikamilisha leo.

Amesema jengo hilo lililoanguka jana asubuhi lilikuwa halikaliwi na watu kutokana na kukabiliwa na uchakavu na hakuna mtu aliyepoteza maisha au kujeruhiwa kufuatia tukio hilo

1 comment:

Anonymous said...

poleni sana ndugu zetu wote mliopo home.na mliopanga katika majengo hayo na mnaoishi humo ondokeni kwa sababu majengo hayo yamesatiliwa dhulma na fisadi anajulikana kuyauza kwa watu wamrima maeno hayo.uislam unakataza dhulma,ondokeni dhulma isije ikakupateni ambao haiwahusu wache mafisadi wenyewe waipate.

na kidogo nataka kuchangia.


Tunapoambiwa Mji mkongwe basi serikali hutumia kiini macho kuwadanganya wananchi kuwa tunauwacha kama ulivo utoe ladha halisi ya mji mkongwe huu ni unafiki na wanakula pesa za unesco bure nitatoa mfano:

Akropolis (Pathenon )Athens) ni jengo lililojengwa 447 BC , Na hadi leo ni kivutio kikubwa cha watalii kwanini?

Kwa sababu linaboreshwa na njia moja ni wanatumia udongo ule ule uliojengewa ambao unapatikana kisiwa kimoja cha Greece,na ukienda ni kama jipya tu? sasa ije kuwa sie majengo ya 1900’s?

poleni sana ndugu zetu huko home Allah atakuvueni salaama salimin.