
Kamati hiyo imepitisha hoja ya kufanywa uchunguzi dhidi ya tuhuma za uhalifu dhidi ya binaadamu nchini Korea Kaskazini.
Ripoti ya tume ya uchunguzi ya umoja huo ilitangaza mapema mwaka huu kwamba kuna ukiukaji mkubwa wa haki za binaadamu Korea kaskazini kushinda muda, uzito na tishio la ukiukaji katika nchi nyengine yote.
Ripoti hiyo imeeleza kwamba mfumo wa magereza Korea kaskazini ni mmoja unaoangamiza, kuua, kuwageuza wafungwa kuwa watumwa, ulio na unyanyasaji, ubakaji na uavyaji wa lazima wa mimba.
Lakini kwa kiongozi anayesimamia mfumo huo, Kim Jong-un, kuishia katika mahakama hiyo ya kimataifa ya uhalifu, italibidi baraza la usalama la Umoja wa mataifa kukubali kuchukua hatua hiyo, na hilo ni jambo ambalo huenda lisishuhudiwe kutokana na kura za turufu za China na Urusi.
Hatahivyo, Korea kaskazini ina wasiwasi. Wanadiplomasia wake wamekuwa wakiwashinikiza waandishi na wanadiplomasia wengine, wakisema kwamba rekodi yao ya haki za binaadamu sio mbaya kama inayotajwa. Na pia nchi hiyo inatishia kufanya majaribio mengine ya silaha zake za nyuklia iwapo kutakua na hatua zaidi dhidi ya uongozi wa nchi hiyo.-BBC
1 comment:
habari inahusu North Korea, kichwa cha habari kinasema korea ya Kusini. just wandering....
Post a Comment