Advertisements

Thursday, November 20, 2014

MAHAFALI YA 12 CHUO KIKUU ZANZIBAR (ZANZIBAR UNIVERSITY)

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Mh. Haroun Ali Suleiman (katikati),akiwa na baadhi ya uongozi wa Chuo Kikuu Zanzibar wakati wa mahafali ya 12 yaliyofanyika katika viwanja vya chuo hicho Tunguu Wilaya ya Kati Unguja.
WAHITIMU wa fani mbalimbali katika mahafali ya 12 ya Chuo kikuu cha Zanzibar (ZU),wakiwa kwenye gwaride lililoandaliwa kwa ajili ya kuwatunuku shahada mbalimbali huko katika viwanja vya chuo hicho Tunguu jana.
BAADHI ya wazee wa wanafunzi wa Chuo kikuu Zanzibar (ZU) wakiwa katika uwanja wa mahafali ya 12 wakihudhuria mahafali hayo yaliyofanyika huko Tunguu.
BAADHI ya wazazi wa wanafunzi wa Chuo kikuu Zanzibar (ZU) wakiwa katika uwanja wa mahafali ya 12 wakihudhuria mahafali hayo yaliyofanyika huko Tunguu.
SPIKA wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mh.Pandu Ameir Kificho (kushoto),akiwa na baadhi ya uongozi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar wakati wa mahafali ya 12 yaliyofanyika chuoni huko, wapili kushoto Makamu Mkuu wa chuo hicho Pr.Mustafa Roshash. Picha zote na Abdallah Masangu

No comments: