Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Bwana Kyle Peters amefanya ziara katika kijiji cha Buma wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani ambako ameshuhudia walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na TASAF na kuridhishwa kwake na namna mpango huo ulivyowanufaisha walengwa ambao wameanza kuondokana na umaskini.
Akiwa kijijini hapo Bwana Peters alitembelea moja ya nyumba iliyoboreshwa na mmoja wa walengwa wa Mpango wa Kunusuru kaya maskini Bwana Bakari Rajabu Bakari ambaye kwa kutumia fedha za ruzuku kupitia Mpango wa kunusuru kaya maskini ameweza kuboresha maisha yake ikiwa ni pamoja na kununua Luninga(TV) huku akimudu pia kusomesha watoto wake.
Bwana Peters amesema utekelezaji wa Mpango huo umeanza kuonyesha mafanikio nchini TANZANIA jambo ambalo litatumiwa na Benki ya Dunia kuendelea kuufadhili huku mfano huo ukisambazwa katika nchi nyingine ili kazi ya kuutokomeza umaskini iwe na mafanikio.
Akizungumza katika ziara hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga amesema mafanikio ya utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya maskini yanatokana na taasisi yake kuamini na kutekeleza majukumu yake kwa uwazi na kuwashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo walengwa katika hatua za utekelezaji wake.
Zifuatazo hapo chini ni baadhi ya picha za ziara ya makau huyo wa Rais wa Benki ya Dunia katika kijiji cha Buma wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
No comments:
Post a Comment