ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, November 2, 2014

MAKONDA AMTWANGA CHUPA WARIOBA LIVE BILA CHENGA

Polisi na watu wengine wakijaribu kumtuliza jaji Warioba baada ya kupigwa chupa na Makonda kwenye mdahalo wa katiba uliofanyika leo na baadae kuvunjika kutokana na vurugu hizo.

Jaji Wariba akitulizwa na baadhi ya watu na polisi aliyekuwepo hapo kwenye mdahalo wa katiba uliofanyika leo Jumapili Novemba 2, 2014 jijini Dar.


Watu wakipata na mshangao wakijiuliza maswali mengi yasikua na majibu

Palikua patashika nguo chanika

Kwa upande wake Gwiji La masuala ya habari nchini na Mhariri wa Gazeti la Tanzania Daima Edson Kamukara alichukizwa na kitendo cha Makonda haya ndio aliyoyasema kwenye ukrasa wake facebook

SOMA ZAIDI WALICHOKISEMA WADAU JUU YA TUKIO HILO LA TUHUMA ZA MAKONDA KUMPIGA WARIOBA NA CHUPA

Kwa upande wake Butiku haya ndio haliyoyasema kuhusu Makonda
Tokea nizaliwe sijawai kukasirishwa na hili jambo la Makonda kumpiga
na chupa Mzee Warioba. Ni utovu wa nidhamu, ni dharau, ni ujinga, ni utoto, ni ukora, ni u.p.mbavu, ni akili ndogo, ni kukosa hekima na misamiati ya namna hiyo kwa hili jambo la Makonda kumpiga na chupa mzee Warioba. Nilikuwepo kwenye eneo la tukio kwa macho yangu nikashuhudia Makonda akimpiga na chupa mzee Warioba, nimeumia sana sana. CCM lazima waruhusu mawazo mbadala ili kujenga Taifa na kamwe kundi moja lenye mawazo yanayofanana hauwezi kujenga Taifa, lazima kuwepo na mawazo huru kwa pande zote katika jamii.


Ila nasita kusema kama kweli Makonda katumwa na CCM inawezekana kabisa katumwa na Nape au Sita. Warioba ni Kiongozi mstaafu tena katumikia Tanzania kwa moyo wote hivyo vijana kukosa adamu mpaka kufikia hatua ya kumpiga na chupa ni ujinga wa hali ya juu na vijana wa pande zote lazima tukemee hili jambo. Jeshi la polisi tafadhali mlifanyie hili kazi, na Makonda naomba nikupe ujumbe kuwa vijana hatutakaa kimya lazima tutakufanya kwa njia yoyote ile uweze kumuomba Mzee Warioba radhi na taifa kwa ujumla, Leo umefanya kwa Warioba, Kesho utasita kufanya kwa Mwinyi au Malecela au Mkapa...

Nimeuzunishwa sana na hili jambo....Shame on you Makonda

Ocampo four

Maneno ya Butiku naomba kunukuu "Huu uhuni uliyofanywa na Makonda haukubaliki hata kidogo, kitendo cha kumpiga Warioba na chupa tunaomba serikali iliangalie jambo hili na pia kuhakikisha katika midahalo mingine huyu muhuni asiwepo, Asanteni" mwisho wa kunukuu.


Maneno ya Butiku baada ya kikao kuisha akiongea na vijana nje ya ubungo plaza


Naomba kunukuu "Kamwe vijana wa CCM msikubali kuchagua viongozi wanaomtuma Makonda kutenda haya, ni uhuni na ujinga wa hali ya juu" alipoulizwa ni nani wako nyuma ya Makonda, bila kusita akasema Membe na Sita
Habari kwa hisani ya Aloyson

2 comments:

Anonymous said...

Dayumnnnnnn haibu zao MAFISADI

Anonymous said...

Alipigwa na chupa gani jamani? Ya kioo au ya plastic?