ANGALIA LIVE NEWS

Monday, November 3, 2014

MAKONDA: SIKUVURUGA MKUTANO WA TAASISI YA MWALIMU NYERERE

Katibu wa Uhamasishaji Umoja wa Vijana wa CCM, Paul Makonda akionesha kwenye simu yake picha ya video iliyopigwa wakati wa vurugu zilizotokea wakati wa mdahalo wa kujadili raismu ya Katiba inayopendekezwa, kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza jana, ambapo Makonda aliyedaiwa kumpiga aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Waziri Mkuu wa zamani Jaji mstaafu Joseph Warioba, amekanusha kumpiga leo katika mkutano wa waandishi wa habari, Dar es Salaam. Pia Makonda amesema kuwa hawezi kabisa kudiriki kumpiga kwani anamheshimu kama babake mzazi. Amesema kuwa hata leo asubuhi amezungumza na warioba kwenye simu kumjulia hali. Warioba naye amekanusha kupigwa na Makonda wala mtu yoyote kwenye vurugu hizo.

Makonda akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) huku akionyesha moja ya magazeti yaliyoandika vurugu za jana.


Waandishi wa habari wakisikiliza taarifa ya Makonda (hayupo pichani).


(Patrick Bozohera na Gabriel Ng’osha/GPL)
KATIBU Mwenezi Idara ya Hamasa na Chipukizi ya UVCCM, Paul Makonda, amekana kuhusika katika vurugu zilizotokea jana katika mdahalo wa Katiba Iliyopendekezwa ambao ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere chini ya Mwenyekiti wake Joseph Butiku.

Hayo ameyasema leo katika hoteli ya Protea, Osterbay, jijini Dar es Salaam alipokutana na waandishi wa habari.

Mkutano huo ulikumbwa na vurugu wakati aliyekuwa mwenyekiti wa kuratibu katiba mpya, Jaji Joseph Warioba, alipokuwa akiwasilisha mada yake, katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.

3 comments:

Anonymous said...

Eeeed makonda ulaaniwe.

Anonymous said...

kila kitu kinaonekana live unabwabwaja nini hapo, akawadanganye wazazi wake makonda sio sis watanzania wa leo

Anonymous said...

Kitendo walichomfanyia mzee warioba ni cha kusikitisha ,wahusika wachukuliwe hatua za kisheria na walaaniwe,