
1. Mohamed Malolo wa Kijiji cha Naipanga
Umefanya mambo gani katika kuinua sekta ya elimu tangu uingie madarakani 2005 hadi sasa?
Jibu: Wakati naingia madarakani mwaka 2005 shule za sekondari zilikuwa sita lakini sasa zipo 19. Nimejenga bweni moja shule maalumu ya wasichana wanalala wanafunzi 45.
Nimeanzisha Mfuko wa Elimu wa Mbunge ambao umesomesha jumla ya wanafunzi 176 ambao ni yatima na wenye kipato duni. Ofisi yangu ya jimbo tangu 2006 imewatafutia ajira ya ualimu hasa wale wote waliosomeshwa na Mfuko wa Elimu wa Mbunge jumla yao ni 148 (2006/2013).
2. Shamzia Ulei, Lucas Aidani, Hadija Mohamed, Venancia Millanzi wote wakazi wa Naipanga
Jibu: Kutokana na tamko la Mheshimiwa Rais, vijiji vyote vilivyopo kandokando ya bomba kuu la maji Mbwinji ikiwamo Naipanga, vitapatiwa huduma ya maji. Ili kuondokana na tatizo la maji, Kijiji cha Naipanga pia kimepatiwa mradi wa kisima kirefu ambao utagharimu Sh36.5 milioni.
3. Mohamed Malolo wa Kijiji cha Naipanga
Umefanya nini katika kudhibiti bei ya korosho?
Umefanya nini katika kudhibiti bei ya korosho?
Jibu: Kwa ujumla ununuzi wa korosho katika mikoa ya Kusini Mtwara, Lindi, Ruvuma (Wilaya ya Tunduru) na Pwani umekuwa na changamoto mbalimbali kama vile kukosa soko la nje, wanunuzi wa ndani kugomea bei dira ya Serikali.
Niliwashauri wabunge wenzangu wa wilaya za Liwale na Ruangwa kwa pamoja tulimshauri Waziri wa Kilimo, Ushirika na Masoko, Christopher Chiza kwamba wananchi wa wilaya hizo tatu wameamua kujitoa uanachama chama kikuu cha Ilulu hatimaye wilaya zetu tatu zimeanzisha chama kipya cha Runali.
4. Asha Linani, mkazi wa Majengo ‘J’
Umefanya nini kukabiliana na tatizo la upungufu wa dawa katika hospitali ya wilaya na zahanati vijijini?
Jibu: Kwa nyakati tofauti, nimekabidhi dawa ambazo zimetumika kutibu magonjwa mbalimbali hadi vijijini. Nimekabidhi vitendea kazi kama vitanda vya kujifungulia kina mama wajawazito, makabati, viti, glovu, viti vya wagonjwa (wheel chairs) n.k. Kwa kutambua na kuthamini afya za wanachi wa jimbo langu, nimekabidhi mabati 80 na saruji mifuko 40 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati mpya Kijiji cha Nakalonji.
5. Selemani Salumu mkazi wa Majengo ‘A’
Ulitoa ahadi ya barabara kuwekwa lami kutoka Nachingwea – Masasi, Nachingwea – Nanganga? Mbona kimya?
Majibu: Sijatoa ahadi ya kuweka lami kama mtoa hoja anavyosema. Nafurahi kusema kwa kiasi kikubwa nimeweka msukumo na kufanikiwa kuishawishi Serikali kuingiza katika mpango wa kuzijenga kiwango cha lami.
6. Nurdini Hashimu mkazi wa Naipanga
Hujatembelea Naipanga tangu uchanguliwe kwa nini?
Jibu: Siyo kweli. Katika vipindi vyote viwili nimekuwa nikishirikiana na wananchi walionichagua katika shughuli mbalimbali za maendeleo bila ya kujali itikadi zao za chama, dini zao, jinsia na maeneo waishio.Kwa mantiki hiyo, ikiwamo Kata ya Naipanga vijiji vyake vyote kama Chiumbati, Chiwindi na Rahaleo nimevitembelea. Hata hivyo, nawakumbusha wananchi wa Naipanga kuwa jimbo la wilaya yetu lina kata 32, vijiji 126 wakati wowote nitawatembelea tena.
7. Said Mfaume wa Kijiji cha Naipanga
Ni kitu gani unajivunia katika kipindi chote ulichoongoza Jimbo la Nachingwea?
Jibu: Heshima na dhamana kubwa mliyonipa ya kuwa mbunge wenu kuanzia mwaka 2005-2010 (awamu ya kwanza) na 2010 – 2015 awamu ya pili kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi.
8. Hadija Mohamedi wa Kijiji cha Naipanga
Una ahadi gani kwa wapiga kura hata baada ya kuwa ametumikia kwa miaka tisa?
Jibu: Ninayo furaha na kuwahakikishia kwamba kwa pamoja, tutaendelea kushirikiana katika kukabiliana na changamoto za elimu, afya mawasiliano ya babarabara na simu, kilimo, vikundi vya wajasiriamali, madhehebu ya dini, vijana, kina mama, wazee bila kujali itikadi za kisiasa, dini, rangi, jinsia au maeneo ya kuishi.
Ni imani yangu mengi mnayajua ambayo kwa muda mrefu yalikuwa ni tatizo lakini hivi sasa kuna mafanikio makubwa kama vile Tarafa za Kilimarondo ambayo sasa tatizo la mawasiliano ya simu limekwisha minara tayari imejengwa wanapiga simu saa 24 kwa siku.
9. Mfaume Nyundo wa Naipanga
Kwa nini hajashughulikia manyanyaso ya wakulima ili kuwakomboa?
Jibu: Msimu wa mwaka 2012/2013 ununuzi wa korosho ulikuwa siyo mnzuri, wakulima hawakupata malipo stahili kutokana na uongozi mbaya wa Ilulu ambao uligubikwa na wizi na ubadhirifu wa fedha. Kitendo ambacho kilisababisha migogoro mingi.
Nimelishughulikia na msimu wa 2013/2014 ununuzi ulikuwa mzuri na wakulima wamelipwa jumla awamu tatu pamoja na bonasi.
10. Davis Osward mkazi wa Rahaleo,
Umefanya jitihada gani kushugulikia tatizo la upungufu wa watumishi wa afya katika zahanati jimboni kwako?
Umefanya jitihada gani kushugulikia tatizo la upungufu wa watumishi wa afya katika zahanati jimboni kwako?
Jibu: Nimeanzisha mpango maalumu wa kutatua tatizo la upungufu watumishi Idara ya Afya Wilaya ya Nachingwea. Nimeanza kuwasomesha kwa kuwalipia gharama za masomo vijana 11 Chuo cha Uuguzi Nachingwea (NTC) kila mmoja amelipiwa Sh1.5 milioni. Wote wamepata ajira wanafanya kazi katika zahanati zilizopo Wilaya ya Nachingwea.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment