Ni ya Twaweza aliyoshika nafasi ya tano

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Bernard Membe.
Twaweza Jumatano iliyopita ilitoa ripoti ya utafiti, pamoja na mambo mengine ikionyesha baadhi ya majina ya wagombea urais wanavyokubalika kwa wananchi ikiwa uchaguzi wa rais ungefanyika Septemba mwaka huu.
Katika orodha hiyo, Membe alishika nafasi ya tano kwa kupata asilimia tano, huku akitanguliwa na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa aliyeshika nafasi ya kwanza kwa kupata asilimia 13; Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (asilimia 12); Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa (asilimia 11); Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba (asilimia 6).
Waliomfuatia Membe ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta aliyepata asilimia nne; Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli waliofungana kwa kupata asilimia tatu pamoja na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe aliyepata asilimia moja.
Aidha, Membe alisema, tafiti zimefanyika mapema kabla ya wakati kufika na bila kuzingatia misingi kanuni na sera za kiutafiti na kwamba zinaweza kuichonganisha nchi na dunia.
Membe ambaye ni miongoni mwa vigogo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaotajwa kutaka kuwania nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu wa mwakani, alitoa kauli hiyo wakati akizungumza katika mahojiano maalum na waandishi wa habari wilayani Kilwa, mkoani Lindi, mwishoni mwa wiki.
Alisema kila kipindi cha uchaguzi kokote duniani unapokaribia kuna kuwa na tafiti ambazo hutoa muelekeo wa nchi kuhusiana na uchaguzi huo, hivyo ni jambo jema.
Hata hivyo, alisema utafiti wa Twaweza haukuwa wa kisanyansi kwani haukubainisha vigezo vya takwimu hizo kulingana na sifa ya waliyofanyiwa tafiti.
“Hata ukiniuliza hapa mimi ni kwanini nimepata asilimia tano au saba sielewi ni vigezo gani vilivyotumika nikapewa, kitu ambacho siyo cha kawaida kwa wafanya tafiti duniani kote. Pili, utafiti kama huu unaweza kuitenga nchi na dunia, kuwafanya wawekezaji ambao tayari ni wawekezaji kupata mashaka kuwekeza kutokana na takwimu hizi za nani anatwaja kuwa rais,” alisema Membe.
Alisema dunia inaweza kuchukulia matokeo hayo na kuyafanya ya kisayansi kumbe utafiti haukutumia kanuni na sifa za wagombea.
“Maoni yangu kwa watu wote ambao wanafanya tafiti wasifanye makosa ya ajabu au watu kuingilia tafiti nchi inaweza kuwekwa pabaya, mimi mwenyewe ni mtafiti na nimeshafanya tafiti tatu najua,” alisema Membe.
Alifafanua kuwa kitendo cha Twaweza kufanya tafiti bila kuhusisha wanaotajwa wote katika kuwania nafasi za urais ni udhaifu wa kitafiti.Alisema pia hata kama walihusisha walipaswa kupewa matakeo yao wote bila kuzingatia kuwa walipata asilimia ngapi.
“Inawezekana vipi ukafanya tafiti za urais leo ukawaacha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (Uratibu na Mahusiano), Stephen Wassira; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof. Mark Mwandosya, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahan Kinana, na wengine wengi takribani tuko 15 hadi 16,” alisema Membe.
Alisema kuna makundi ya wanawake ambayo wapo kama Spika wa Bunge, Anne Makinda, Waziri wa Sheria na Katiba, Asha-Rose Migiro walitakiwa kuhusishwa wote.
Alifafanua kuwa Kinana anazunguka nchi nzima, hivyo haiwezekani wasiwapo watu wa kumtaka awanie nafasi ya urais hata kama hataki.
Membe pia alihoji sababu za utafiti huo kutowahusisha Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Mchemba; Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harisson Mwakyembe na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba.
“Twaweza walitakiwa kusema ndani ya CCM wanaotajwa wangeuliza nani anafaa kwenda tano bora, tatu bora ni akina nani na kisha sifa ya kiongozi bora, huo ndiyo utafiti bila kuacha matokeo ya hata mmoja. Mfumo ambao sisi CCM tunautumia 5,3,1,” alisema.
Alisema utafiti wa mtu yoyote ambaye hafuatilii kanuni ya 5,3,1 utapotosha watu, lakini hata ukipatia ni kwa kudra za Mungu.
Aidha alisema anashangazwa na kitendo cha Twaweza kutohusisha matokeo haya ya tafiti na rushwa ambayo katika tafiti zake za miezi mitatu iliyopita zilionyesha rushwa ni kero kubwa.
“Twaweza hii si mara ya kwanza kutoa utafiti. Miezi mitatu iliyopita waliwauliza Watanzania ni kero gani inawasumbua, walisema rushwa na safari hii rushwa haipo nina mashaka na tafiti zao kuwa kwa kipindi hiki cha miezi mitatu rushwa imetoweka?” alihoji na kusema siyo kweli.
.Kuhusu rushwa, alisema: “Mimi sijawahi kutoa rushwa, naapa mbele za Mungu sijatoa rushwa ya aina yoyote ile.” Alisema hata uchaguzi mkuu wa CCM wa mwaka 2012 aligombea ujumbe wa Halmashauri Kuu ta Taifa (NEC) na alishinda kwa asilimia 71, hakutoa rushwa.
“Nilienda kujaribu tu katika uchaguzii ule ili nijue nafasi yangu, na bahati nzuri nikashindwa nafasi ya sita, kuna watu walihusishwa na rushwa, lakini mimi sikutoa shilingi moja na kama yupo anayesema nilitoa rushwa aseme,” alisema.
Alisema sifa bora ni kuchaguliwa bila kushinikiza watu katika maeneo yoyote kwa kutumia fedha.
LINI ATATANGAZA NIA YA KUWANIA URAIS
Alisema anatarajia kutangaza nia yake ya kugombea urais pindi muda utakapofika ila kikubwa anachosubiri ni kutimia kwa ndoto zake ambazo mpaka sasa ameshaota mbili, zinazosubiri mnajimu azitafsiri.
Alisema, kuwania nafasi kubwa kama hiyo ambayo inatoa hadi mamlaka ya kutoa roho ya mtu unahitaji hekima ya Mungu katika kukuongoza kuomba nafasi hiyo.
“Ninaendelea na kulitafakari siwezi kukurupuka, nilisema nasubiri kuoteshwa nimeshaoteshwa ndoto mbili hivi karibuni, ninachosubiri ni mnajimu aweze kunitafsiria,” alisema Membe.
Alisema siyo mtu yeyote ambaye anaona ana uwezo wa kuzungumza na kuahidi jambo fulani anaweza kuongoza bali yule mwenye sifa na vigezo vinavyoendana na chama.
“Uongozi ni vigezo, lazima tuwe na watu wenye uwezo kwa kuzingatia vigezo ambavyo ndivyo vinampa mtu sifa za kuwania nafasi,” alisema.
Alifafanua kuwa, sifa na vigezo ndizo zinazompa nafasi mtu kugombea kwa sasa si nani anakuahidi nini ndiye kiongozi bali ni kiongozi ambaye anatakiwa kubeba roho za watu milioni 45.
“Si suala la elimu, maji, barabara, umeme bali ni lazima sifa za uongozi ndizo zinakupa kigezo cha kuwa kiongozi, ukisema kuahidi hata mbabe naye anaahidi anasema haya yote, lakini je, unasifa?” alihoji Membe.
Alisema kuongoza taifa si jambo la kushabikia bali ni kutwishwa mzigo mkubwa na ukikosa si lazima ujutie na kwamba kiongozi si kiongozi wa chama tena bali chama ndiyo kitakuwa watenda kazi wake, hivyo ni kuwa na busara kubwa.
JE, ANAFAA KUWA RAIS?
Alipoulizwa kama ana sifa za kugombea urais, alisema ni jambo zito kusema kama anafaa ama la, ila anahitaji kutafakari kabla ya kulizungumzia.
“Nashangaa leo kuona watu wanaona urais wa kubeba uhai wa Watanzania wote hawa kama udereva wa gari ambao unaweza kufundishwa na dereva mwenzako, ni cheo cha juu sana, unabeba uhai wa nchi, hata wewe mwandishi ukiambiwa sasa hivi hapa wewe ni rais unaweza ukazimia,” alisema Membe.
KUTANGAZA NIA
Alisema yeye hajatangaza kwa sababu ana majukumu ya kumalizia kazi ya rais aliyepo madarakani.
“Kama ningetangaza mapema nisingeweza kumudu majukumu yangu ya kazi na siamini kama waliyowahi kutangaza wanaweza kuwa washindi, nafikiri wao wanajimudu kufanya kazi zao na jukumu la kusaka urais,” alisema Membe. Alifafanua kuwa, ukianza kutangaza sasa unaweza kusahau kazi moja na kuukaacha kazi ya pili, jambo ambalo unaweza ukapoteza kiwango cha kazi.
“Wengi walioko wasio na kazi (job less) ni rahisi kutangaza maana huna kazi ya kufanya. Ni sawa na wewe nimekuajiri halafu unasema unahama mwezi ujao, kwa mtu mwenye kazi lazima upime vizuri,” alisema Membe na kuongeza kuwa kama una nguvu za ziada na unaweza kufanya kazi mbili kwa wakati mmoja.
KUHUSU UBUNGE
Kuhusu kugombea ubunge, alisema hana mpango tena wa kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo lake la Mtama.
Alisema aliahidi kuwa ameongoza vipindi vitatu katika jimbo hilo na kuwa aligombea kipindi cha tatu baada ya kuombwa na wananchi wake.
Alisema takwimu za ushindi wake katika ubunge zimekuwa zikipanda kila awamu na kwamba kwa kipindi cha kwanza mwaka 2000 alipata asilimia 77, 2005 (asilimia 82) na 2010 asilimia 87.
“Sitaweza kutumia tena nchi kwa ubunge, nimekaa kwa miaka 15,” alisema.

CHANZO: NIPASHE
1 comment:
Kwanza napenda kukushukuru sana Mheshimiwa Membe kwa kuwa muwazi. Pili, kwa uelewa wangu wewe ni mkristo wa Kanisa Katoliki, hivyo kwa mkristo yeyote uhitaji mnajimu. Mnajimu wa nini kwako mkristo? Ushauri wangu wa bure, unatakiwa usome Biblia kwa bidii huku ukimuomba MUNGU, ikiwezeka ujitahidi kufunga. BWANA YESU, atakutafsiria. Usijenge imani yako kwa wanadamu, jenga kwa MUNGU. Nami nakuunga mkono ukithibitisha kuwa ni MUNGU amepanga, yeye atakuongoza na kupigania. Amen.
Post a Comment