Mashabiki Yangawakishangilia ushindi wa goli 2 huku wakionyesha vidole viwili juu katika mtanange wale Taifa kati ya timu ya Mgambo JKT kutoka Tanga na Yanga ya Dar es Salaam na timu ya Yanga kuibuka na pointi zote 3 baada ya kuifunga timu hiyo ya wagosi wa kaya kwa bao 2-0.
Ni raha tu kama wanavyoonekana mashabiki wa Yanga walioshuhudia timu hiyo ilipoibanjua Magambo JKT kwa bao 2-0 kwa mechi iliyochezewa uwanja wa Taifa.
Kipa wa Mgambo JKT, Said Lubawa, akilalamika baada ya Msuva kuutundika mpira wavuni kuandika bao la kwanza kati ya mawili ambayo Yanga ilishinda
Winga wa Yanga Simon Msuva, akishangilia bao lake
Mwamuzi Ngole Mwangole kutoka Mbeya, akimuonyesha kadi Nyekundu, mlinzi wa Mgambo JKT kutoka Tanga, Nasoro Gumbu, baada ya kumchezea vibaya Mrisho Ngasa wa Ynga
Mrisho Ngasa wa Yanga, (Kushoto), akiwatoka walinzi wa Mgambo JKT, Bushiru Mohammed, (Wapili kulia), na Ramadhan Malima
Mrisho Ngasa akipambana vilivyo na mlinzi wa Mgambo JKT
Adha ya kufungwa, mlinzi wa Mgambo JKT, akionyesha kuhuzunika na kichapo cha Mabao 2-0 mbele ya Yanga
Mshambuliaji wa Yanga, Continho, akijaribu kumtoka mlinzi wa Mgambo JKT
Kocha mkuu wa Mgambo JKT, Bakari shime akitafakari, wakati tayari timu yake iko nyuma kwa bao 1
"Wakati ukuta" Kocha wa Mgambo JKT, Bakari Shime, akitazama saa yake, huku kulia akitafakari mbinu gani ya kuinasua timu yake dhidi ya Yanga
Mshambuliaji wa kati wa Yanga, Mbrazil Jaja, (Kushoto), akijaribu kumtoka mlinzi wa JKT, Malima
Kocha mkuu wa Yanga, Macio Maximo, akiwapongeza wachezaji wake, kwa kufanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mgambo JKT kutoka Tanga
Macio Maximo
Continho, akipiga hesabu zake Picha kwa hisani ya K-VIS





















No comments:
Post a Comment