Jaji Joseph Warioba akitoa mada.
Mtoa mada katika mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekezwa, Jaji Joseph Warioba akitoa mada kabla ya mkutano huo kuvunjika katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Saam leo.
Baadhi ya vijana walioingia na mabango ndani ya ukumbi wa mkutano wakiwa na mabango yaliyokuwa yakisomeka ‘Katiba inayopendekezwa tumeipokea tunaiunga mkono’.
Mlinzi wa Jaji Joseph Warioba (kushoto) akimkinga kwa mikono ili asipate madhara baada ya mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekezwa kuvamiwa na kundi la vijana na kusababisha uvunjifu wa amani.
Jaji Joseph Warioba akiangalia usalama wake kabla ya kuondolewa mlinzi wake katika ukumbi wa Ubungo Plaza ambapo mdahalo wa kuijadili Katiba inayopendekezwa ulikuwa ukifanyika kabla ya kuvunjika.
Aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Humphrey Polepole akimzuia mmoja wa vijana aliyekuwa na jazba mara baada ya kutokea kwa vurugu katika mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekeza.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), Joseph Butiku (katikati) akisindikizwa kuingia katika chumba cha VIP mara baada ya kuvunjika kwa mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekezwa. Mdahalo huo uliandalia na taasisi hiyo.
Vijana wakiwa na mabango.
Mabango yakiwa juu.
Vujo zinaanza.
Mmoja wa vijana waliokuwa wakitoa maneno ya kashfa kwa Jaji Warioba akiwanyooshea vidole viongozi wa meza Kuu.
Baadhi ya viti vilivyovujwa.
Jaji Warioba akitoka katika ukumbi huku akisindikizwa na askari kanzu.
Jaji Warioba akisindikizwa na makachero wa Polisi.
Jaji Warioba akiwapungia mkono wananchi waliokuwa wamefurika nje ya jengo la Ubungo Plaza ambako mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekezwa ulikuwa ukifanyika.
Wananchi walikuwa nje ya jengo la Ubungo Plaza wakimshangilia Jaji Warioba wakati akitoka katika ukumbi wa mdahalo huku wakimuita 'Rais Rais'.(Picha zote na Francis Dande).
6 comments:
Shame on CCM...yani sasa this is too much...mzee huyu ni one of the best,hard working and hana ufisadi na the new CCM imejaa ufisadi na ubabe wakijinga....mfano huo hapo ...jamani time kuwaondoa hawa CCM maana hatuelekei pazuri
Geee am lost. This old man is one of the honest leaders I have ever seen. Nyie vijana mnaotumwa, mwacheni huyou mzee. Hiyou katiba siyou mawazo yake bali mawazo ya wananchi. Yeye alikusanya. Shame on you called "youth". Leave the mzee alone.
I agree na mdau hapo juue.
Ni jambo la aibu sana. ccm naomba mkubaliane na mabadiliko. watu wa sasa ni waelewa na wana uhuru wa kufanya maamuzi na sio ubabe ambao nyie mnataka kufanya.
hao vijana wapelekww Mirembe Dodoma kupimwa akili!! Mzee Wariobal hawezi hata kuua mbu jinsi alivyo safi na ni mkweli 110%.
That is an assault and it is a criminal offence which carries 10 years plus if it was done where I am. But in Tanzania itaishia hapo hapo.
angalia msije mkatuulia Warioba wetu mtetezi wa wanyonge CCM acheni ubabe huo ubabe una mwisho.
Why kuilaumu CCM?? Hawa vijana hawajulikani ni wa chama gani!!!
Post a Comment