Advertisements

Sunday, November 23, 2014

SERIKALI YAJIDHATITI KUKABILIANA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI KATIKA SEKTA YA ELIMU CHINI.

Naibu Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Mhe. Angellah Kairuki (kushoto) akiwahutubia wahitimu wakati wa Mahafali ya Tisa ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere siku ya tarehe 22 Novemba, 2014 jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Shadrak Mwakalila.
Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Shadrak Mwakalila.akiwahutubia wahitimu wakati wa Mahafali ya Tisa ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere siku ya tarehe 22 Novemba, 2014 jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wahitimu wa ngazi mbalimbali wakifuatlia hotuba toka kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Mhe. Angellah Kairuki wakati wa Mahafali ya Tisa ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere siku ya tarehe 22 Novemba, 2014 jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wahitimu wa ngazi mbalimbali wakifuatlia hotuba toka kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Mhe. Angellah Kairuki wakati wa Mahafali ya Tisa ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere siku ya tarehe 22 Novemba, 2014 jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wahitimu wa ngazi mbalimbali wakifuatlia hotuba toka kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Mhe. Angellah Kairuki wakati wa Mahafali ya Tisa ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere siku ya tarehe 22 Novemba, 2014 jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA, MAELEZO-DSM)


Na Benedict Liwenga, Maelezo-DSM.

SERIKALI imekuwa ikifanya jitihada za dhati katika kukabiliana na changamoto ya kushuka kwa kiwango cha wahitimu wa kidato cha Nne na Sita katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Mhe. Angellah Kairuki wakati wa Mahafali ya Tisa ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere yaliyofanyika 22 Novemba, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Mhe. Kairuki aliwaeleza wahitimu hao kuwa, katika taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Chuo hicho inaonyesha kuwa idadi ya wahitimu imepungua kutoka wahitimu 919 mwaka jana, hadi kufikia 689 mwaka huu, hali iiyochangiwa na kushuka kwa kiwango cha ufaulu kwa wahitimu wa vidato hivyo vya Sita na Nne.

Alieleza kuwa, Serikali imefanya juhudi za kukabiliana na tatizo hilo kwa kuanzisha Mikakati mbalimbali ikiwemo; Mpango wa Elimu ya Shule za Msingi, Mpango wa Elimu ya Sekondari, Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Ufundi wa miaka mitano (2013/14-2017/18) pamoja na Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa “Big Results Now” (BRN).

Mhe. Kairuki alibainisha kuwa, jitihada hizo zinaonyesha dhamira ya dhati ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutatua ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu nchini.

“Ni matumaini yangu kwamba, juhudi hii za serikali zinazaa matunda na zimeanza kujionyesha kwa kupanda kwa kiwango cha ufaulu katika shule zetu za sekondari nchini, hivyo ni dhahiri kuwa kasi ya udahili katika vyuo vyetu itaongezeka halikadhalika na idadi ya wahitimu kwa siku zijazo”, alisema Kairuki.

Aliwaasa wahitimu wa chuo hicho na kuwataka kujiepusha na tabia hatarishi zinazoweza kuwaharibia maisha yao zikiwemo tabia za ngono zembe pamoja na utumiaji wa madawa ya kulevya.

“Ninawasihi mjiepushe na starehe na tamaa zinazoweza kuwaletea matatizo makubwa, tumieni vizuri elimu mliyoipata chuoni hapa kwa kutunza afya zenu, kuzingatia maadili mema na kutawala nafsi zenu, lakini pia jiendelezeni kitaaluma, msiridhike na viwango vya elimu mlivyonavyo”, aliongeza Kairuki.

Naye Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Shadrak Mwakalila alisema kuwa katika kutekeleza matakwa ya kisheria, hususani Sheria Namba Sita ya mwaka 2005 ya Chuo hicho, chuo kiliweza kukamilisha ujenzi wa Tawi la chuo cha Mwalimu Nyerere upande wa Zanzibar ambapo jengo moja lenye ghorofa Nne katika eneo la Bububu mjini humo lilizinduliwa rasmi na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein siku ya tarehe 18 Mei, 2013 na limeweza kutoa fursa ya kuendesha mafunzo ya ngazi ya Cheti katika Kazi za Vijana na hivi sasa chuo kinatarajia kuongeza programu nyingine za mafunzo katika tawi hilo.

Akizitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili chuo hicho alisema kuwa, kuna uhaba mkubwa wa hosteli kwa upande wa chuo cha Kivukoni pamoja na Tawi lake la Zanzibar, pia kumekuwepo na ufinyu wa bajeti ambao unaathiri utekelezaji wa majukumu ya chuo hicho, na matatizo mengine ni mmomonyoko wa ardhi katika fukwe za Bahari ya Hindi unaohatarisha kuangusha baadhi ya majengo ya chuo hicho.

Katika mahafali hayo, jumla ya wahitimu 689 wakiwemo wanawake 400 sawa na asilimia 58.1 na wanawaume 289 sawa na asilimia 41.9 walihitimu elimu yao katika ngazi za Cheti, Stashahada ya Kawaida pamoja na Shahada ya Kwanza

No comments: