Kulia ni Richard Mchomvu mkuu wa Polisi wilaya ya Mbeya akiwa na jalada la uchunguzi kuhusiana na chuo hicho.
Serikal imekifunga Chuo cha Kilimo na Mifugo cha Nice Dream kilichopo mtaa wa Mapelele Kata ya Ilemi Jijini na kuwataka wanachuo wa chuo hicho kuondoka chuoni hapo baada ya siku tatu.
Agizo hilo lilitolewa na Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Mbeya Bi. Quip Mbeyela aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Daktari Norman Sigala na kwamba Serikali itagharamia chakula kwa siku tatu ambapo Serikali ilikabidhi shilingi laki tatu kwa Mtendaji Kata Bi Gladness Sapuka kwa ajili ya
kununua chakula kwa wanachuo 48 waliokuwa wakisoma katika chuo hicho ambacho hakina usajili kutoka Baraza la Vyuo (NACTE).
Imeelezwa kuwa, wamiliki wa chuo hicho walitumia kwa hadaa jina la Mhe. Frederick Sumaye, kuuaminisha umma kuwa Waziri Mkuu huyo mstaafu ndiye aliyezindua chuo hicho.
Mbali ya chuo hicho kutosajiliwa na NACTE, pia mmiliki wake hafahamiki vyema. Kaimu Katibu Tawala aliambatana na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mbeya Richard Mchumvu ambaye alisema kuwa Jeshi la Polisi linamtafuta mtuhumiwa na kwamba pindi atakapopatikana atafikishwa mahamani ili kujibu tuhuma za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kwa kutumia kivuli cha chuo na kuwatapeli wanachuo 48 waliokuwa na nia ya kusomea taaluma ya kilimo.
Kauli hiyo ilikuwa mwiba kwa wanachuo hao pale Kaimu Katibu Tawala aliposema kwamba Serikali haina chuo cha kuwapeleka kwa kuwa hakuna nafasi katka Vyuo vya Kilimo Mkoani Mbeya na muda wa usajili wa wanavyuo vya kilimo umemalizika.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa hawaamini tamko lililotolewa na Selikari juu ya kufungwa chuo chao
Mbeya Yetu:
|
No comments:
Post a Comment