Advertisements

Saturday, November 22, 2014

Shukurani zetu za dhati

Kamati ya Fundraising ya Rashidi Mkakile. Inawashukuru sana kwa mchango wenu wa hali na mali na moyo mliouonyesha na kuungana nasi siku ya tarehe 16/12/2014 ili kumsaidia ndugu yetu.

Japo kulikua na hali mbaya ya hewa lakini mlijitoa kutusaidia. kiasi cha fedha kilichopatikana tulitangaza siku ya tukio katika ukumbi. Zitamsaidia ndugu yetu wakati huu mgumu wa kuuguzwa.

Tunakushukuruni sana. Mungu awajaalieni nyote.

Tunasema asante sana kwa watanzania wa Boston na wana Massachusetts na state za jirani kwa ushirikiano, upendo na msaada wenu hauna kifani, tunafarijika kwamba Mtanzania ameugua ugenini ila kwa upendo wenu hatukua wageni kwani mnakuja Hopitali kumuona na kumfariji mgonjwa. Hiyo imetupa faraja. Mola awalinde.

Ndugu yetu bado atakuwepo maeneo yenu kwa muda mrefu akiendelea na matibabu hapo msisite kumfariji punde mpatapo nafasi.

Msaada bado unahitajika kwa atakaeweza kupitia
Bank of America account - 4460 3059 3659 (Isca Kauga zip code 20904)
au kwa credit pard/PayPal (Credit/Debit cards are securely processed by PayPal)
Asanteni sana.
Kamati.

No comments: