Advertisements

Sunday, November 2, 2014

Tanzania Karate-Do Federation (TKF).

Kwa niaba ya walimu ma-(Sensei) watano toka Tanzania, Sensei Dudley Mawalla, Sensei Daud Magoma, Sensei Kheri Kivuli, Sensei Edgar Kaliboti na Sensei Rumadha Fundi, tunatowa
shukrani za kupewa dhamana kubwa ya heshima na vyeo vya ngazi za juu toka shirikisho la Karate Tanzania (Tanzania Karate-Do Federation).

Chini ya uongozi wa mwenyekiti Sensei Geofrey Kalonga na katibu mkuu wake Sensei Phillip Chikoko, hatuna budi kuitikia wito wa kuchangia maendeleo ya sanaa ya Karate inayohitaji nidhamu na mifano ya ujasiri wa hali ya juu kwenye kizazi kipya cha taifa letu.
Sensei Dudley Mawalla na Sensei Daudi Magoma, walitunukiwa shahada au Dan ya Saba kila mmoja na Sensei Kheri, Sensei Kaliboti na Sensei Rumadha Dan sita kila mmoja.Sensei Dudley
Mawalla, mwanzilishi wa Japan Shotokan Tanzania.Sensei Kaliboti, mkufunzi wa Gracie Ju jitsu, Australia, Sensei Rumadha, Okinawan Goju Ryu Jundokan KyoKai, Texas, USA, Sensei Daudi na Sensei Kivuli, wakufunzi wa Okinawa Goju Ryu, Dar Es Salaam, Tanzania. 

Sherehe hizo zilifanyika uwanja wa ndani wa taifa
kuadhimisha siku ya baba wa taifa Mwalimu Nyerere, kushirikishwa na zaidi ya wana-Karate 50 wa ngazi mbalimbali toka shule na mikoa tofauti hapa nchini. Wote tulio tunukiwa
heshima hiyo, hatunabudi kusema asante zetu katika shirikisho la Karate Tanzania(Tanzania Karate-Do Federation).
 Kwa picha zaidi bofya soma zaidi


No comments: