ANGALIA LIVE NEWS

Monday, November 24, 2014

TARATIBU ZA TIBA ZA RAIS JAKAYA KIKWETE ZAKAMILIKA

ETETHE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz              

Fax: 255-22-2113425



PRESIDENT’S OFFICE,
      STATE HOUSE,
              1 BARACK OBAMA ROAD,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Taratibu za Tiba za Rais zakamilika
Taratibu za matibabu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, zimekamilika leo, Jumatatu, Novemba 24, 2014.

Taratibu hizo za matibabu za Mheshimiwa Rais Kikwete zimekamilika kiasi cha saa 12 asubuhi ya leo wakati madaktari bingwa katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko mjini Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani, walipomfanyia hatua ya mwisho ya tiba.

Hata hivyo, Rais Kikwete ataendelea kupumzika na kuangaliwa kwenye Hoteli Maalum inayohusiana na Hospitali ya Johns Hopkins kwa siku mbili hadi tatu kabla ya kuanza safari ya kurejea nyumbani.

Kama kila kitu kitakwenda kama ilivyopangwa na madaktari, Rais Kikwete anatarajiwa kurejea nyumbani Jumamosi, Novemba 29, 2014.

Rais Kikwete aliondoka nchini Alhamisi ya Novemba 6, 2014, kwenda kufanyiwa uchunguzi wa afya yake lakini madaktari katika Hospitali ya Johns Hopkins waliamua kumfanyia upasuaji wa tezi dume Jumamosi ya Novemba 8, 2014.

Rais Kikwete anaendelea kuwashukuru Watanzania kwa sala na maombi yao ya kumtakia heri ya kupona haraka na kurejesha afya njema katika kipindi chote cha ugonjwa wake.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.

24 Novemba,2014

3 comments:

Anonymous said...

Ukirudi nyumbani hakikisha kuwa watanzania wanapata matibabu yote yanayohitajika kwa kuwa ni wachache mno wanaoweza kwenda India, South Africa, USA, UK. Pia hospitali zetu ziwe na vifaa na dawa za kutosha. Tunataka haya mambo ya ESCROW, EPA, RICHMOND, RADA na uchafu mwingine wanaohusika wachukuliwe hatua ikiwemo kufungwa jela na kulipa pesa za wananchi. Tumesikia "bwana mkubwa" amehusika, kama ni wewe tunataka
UJIUZULU.

Anonymous said...

Asante kwa taarifa nzuri na tunamwombea aweze kupata nafuu tosha arejee nyumbani. TUNAMUOMBA RAIS CHONDE CHONDE, kama umeshindwa kutoa neon ukiwa huko Amerika matibabuni, tunakutegemea ukirudi nyumbani yaani siku ya kwanza kabisa ofisini asubuhi uzungumze na waTanzania unaowaongoza kuhusu hili sakata la ESCROW linaitia aibu Tanzania na ona jinsi shilingi ilivyoporomokA, UNAYO TIMU MBOVU kwa saana na imekuharivia sana muda wako wa kumaliza madaraka. TUNAKUSUBIRIA NA USIWAGOPE TOA KAULI KAMA RAISI wajiuzulu na fedha zirejeshwe mara moja hakuna ubishani hapa kwani wote wanajulikana lisifunikwe au kufanywa jambo la kisiasa NO NO NO !! DJ L. hili ni chungu kwa waTanzania!! usifunike.

Anonymous said...

Good news, come home JMK and sort out this massive ufisadi which some leaders tried hide. Ni hela zetu Mr President, tafadhalis sana wachukulie hatua kali hawa. I am shocked they are still attending Bunge as if they have done nothing wrong.