Advertisements

Saturday, November 22, 2014

WAHALIFU MTANDAO WATEGEMEWA KUELEKEZA NGUVU ZAO BARANI AFRIKA


Itakumbukwa katika mkutano uliofanyika  mapema mwezi huu  jijini "CAIRO" hofu ya ukuwaji wa uhalifu mtandao unaoweza kurudisha nyuma uchumi wa mataifa ya Afrika  ulipata kujadiliwa kwa kina huku nchi ya Misri ikionyesha washiriki wa mkutano huo jitihada inayoendelea nayo katika kukabiliana na uhalifu mtandao.

Ime ripotiwa na Mtandao wa "MGAFRICA" kuhusiana na kilichojiri katika mkutano uliokamilika jijini Johannesburg, Afrika kusini wa maswala ya usalama mitandao ambapo Bara la Afrika limetabiriwa kuwa na ukuaji wa uhalifu mtandao kutokana na mikakati daifu ya kujiweka salama huku ikiwapatia wahalifu mtandao urahisi mkubwa wa kuleta maafa siku za usoni.

Kumeendelea kuwa na wimbi kubwa la uhalifu mitandao ingawa jitihada za kukabiliana na uhalifu huo zimeendelea  kugharimu mataifa mengi hivi sasa. Mataifa yamekua yakiwekeza kwenye maswala ya usalama mitandao lakini bado wahalifu mtandao wameonekana kuendelea kutamba.

Mkutano huo wa maswala ya  usalama mitandao uliangazia kwa karibu  sababu za ukuaji wa uhalifu mtandao na nini kifanyike kwa mataifa ili kuweza kupiga hatua ya kubaki salama kimtandao. Wataalam wa maswala Mtandao kutoka katika mataifa mbali mbali walikutana  kuyajadili mambo hayo kama ifuatavyo:-

Swala la kukuza uwelewa kwa watumiaji mtandao kuhusu matumizi salama ya mitandao lilionekana bado ni changmoto katika mataifa mengi. Na njia rafiki za kuhakiki kampeni hii ya kuamasisha uma juu ya matumizi salama ilipelekea mambo mengi kuangaziwa macho huku "TOVUTI" maalum kwa ajili ya uelewa wa matumizi salama mitandao ikipata kuzinduliwa.


Sheria nazo zilionekana kua changamoto kubwa sana barani Afrika. Kumekua na kusua sua sana kwa sheria mitandao kuanza kufanyiwa kazi huku Wataalam kutoka katika vyombo vya sharia (Mahakama) wakionyesha hali wanayokumbana nayo katika kutolea maamuzi dhidi ya uhalifu mtandao.

Tulipata kufafanua na kueleza usalama mitandao haunabudi kwenda sambamba na sharia zake maalum zinazopaswa kupitiwa mara kwa mara na kuborehwa ili kuendana na wakati. Bila kufanya hivyo hali ya wahalifu mtandao kufanya matukio na kutopatiwa adhabu stahiki itaendelea kuchangia ukuaji wa uhalifu huu.

Swala la Uhaba wa wataalam nalo halikubaki nyuma. Mjadala mkubwa uliangazia jitihada mbali mbali za mataifa zinazofanywa ili kuweza kuwa na wataalam wakutosha wenye uwezo sahihi wa kujua namna ya kudhibiti, kukabiliana na kuzuia uhalifu mtandao.

Ushirikiano katika maswala ya usalama mitandao kuanzia ngazi ya kitaifa kibara na kimataifa ilionekana bado ni changamoto kubwa sana ambayo bado ku safari ndefu kuhakiki tunafikia malengo. Njia rafiki ya kuhakiki tunakua na utamaduni wa kushirikiana kuanzia ngazi ya taifa moja moja kabla ya kuvuka mipaka ilisisitizwa kufanyiwa kazi ili kurahisisha vita dhidi ya uhalifu mtandao.

Wataalam mbali mbali walipata fursa ya kuonyesha kwa vitendo gunduzi mpya za kisasa zenye kurahisisha uwezo wa kubaini, kuzuia na kukabiliiana na uhalifu mtandao ambapo kila gunduzi ilipata kujadiliwa kwa kina ili kuweza kuleta tija dhidi ya mapambano na uhalifu mtandao.

Mataifa na vikundi mbali mbali pia vilipata fursa ya kuonyesha takwimu mbali mbali za maswala ya uhalifu mtandao na njia mbazo mataifa hayo yameendelea kukabiliana na wimbi kubwa la wahalifu mtandao. Mjadala mkubwa katika kuzikosoa na kurekebisha jitihada hizo ulipata kuonekana wenye malengo madhubuti ya kuwa na bara salama kimtandao.


Pali angaziwa pia vifaa mbali mbali vya kiusalama mitandao ambapo vimeendelea kutumika ipasavyo kuhakiki uhalifu mtandao unakabiliwa ipasavyo. Huku pakitolewa baadhi ya vifaa hivyo kwa washiriki ili kuweza kuongeza tija kwenye mapambano dhidi ya uhalifu mtandao katika mataifa mbalimbali barani Afrika.

No comments: