Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za uzalishaji Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Abdullah Makame akimkaribisha mgeni rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Zanzibar Salum Maulid Salum (kati kati) kufungua warsha ya utayarishaji mkakati Itifaki ya soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki. Wakwanza (kushoto) Makamu wa Rais wa Chamber of Commerce Zanzibar Ali Aboud Mzee.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Zanzibar Salum Maulid Salum akifungua mkutano huo unaofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resourt Mbweni Wilaya ya Magharibi Zanzibar.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria ufunguzi wa Warsha ya utayarishaji mkakati Itifaki ya soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki wakifuatilia ufunguzi wa mkutano huo Zanzibar Beach Resourt Mbweni.
Baadhi ya washirki wa warsha ya utayarishaji mkakati Itifaki ya soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora alipokuwa akifungua warsha hiyo.
Picha ya pamoja ya washiriki wa warsha hiyo na Mgeni rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Salum Maulid Salum (wa katikati) waliokaa.
No comments:
Post a Comment