
Hata hivyo, jana na juzi hali ilikuwa shwari katika eneo hilo huku wakazi wilayani humo wakishuhudia helikopta ya polisi ikiwa na makamishna kutoka Makao Makuu ya Polisi, Dar es Salaam ikizunguka angani kuendelea na ulinzi.
Naye, Mkuu wa Mkoa huo, Eraston Mbwilo akizungumza kwenye kikao cha ushauri cha mkoa, alisema chanzo cha mgogoro wa ardhi na mauaji hayo ya Kiteto yanasababishwa na baadhi ya watu kuhodhi ekari za ardhi bila ya kuwa na vibali. “Hili suala la baadhi ya watu kudai kuwa Kiteto imegeuka kuwa Somalia siyo kweli, mgogoro wa Emboley Murtangos unasababishwa na baadhi ya watu kujimilikisha ekari nyingi za ardhi kiholela,” alisema Mbwilo na kuongeza: “Unamkuta mtu anamiliki ekari zaidi ya 500 kiholela, huu ni ukiukwaji wa sheria, vijiji vina utaratibu wa kugawa maeneo, kwa nini wasiufuate?” alihoji. Alisema kwa sasa hali ni shwari katika eneo hilo na wanaendelea kufanya mazungumzo na viongozi wa jamii ya wakulima na wafugaji ili kuhakikisha kuwa mauaji na vurugu hizo havitokei tena.
No comments:
Post a Comment