Advertisements

Monday, December 22, 2014

AARIFA YA SHEREHE TAREHE 27 DISEMBA 2014.


Ndugu Watanzania,
 
Matarajio yangu natumai munaendelea na afya njema.
 
Kwa niaba ya uongozi wa Jumuiya ya Tanzaseattle, napenda kuwatangazia pamoja na kukuombeni kuhudhuria rasmi kwenye sherehe itakayo jumuisha matukio matatu muhimu kama ifuatavyo:
 
1. Sherehe ya Uhuru wa Tanganyika
2. Sherehe ya Krismas
3.Sherehe ya Makabidhiano majukumu kwa uongozi mpya.
 
  • Tarehe rasmi ya sherehe ni 'December 27th, 2014'
  • Muda rasmi wa sherehe  ni kuanzia Saa 11 jioni hadi riamba(5pm - sunrise)
  • Anuani ya sehemu ya sherehe ni:
 
           411 156th Ave. Ne
Bellevue, Wa 98007.
 
​ 
  • Kwa kuimarisha jumuiya yetu. Uongozi unakuombeni kuchangia kiingilio cha $10 {kwa watu wazima(adult)}.
 Burudani ya muziki kabambe italetwa kwenu na DJ. Haroub, vile vile kutakuwepo na ''Live Band Music Performance' itakayoletwa na kundi la 'Planet Sativa and Fonebug'.
  • Vyakula vyenye ladha murua na vinywaji vyepesi vitakuwepo bila malipo.
 
Tafadhali musikose kuhudhuria shughuli hii muhimu ya Jumuiya. Kwa uchache wa muda munaombwa kusaidia kusambaza taarifa hili kwa kila Mtanzania na marafiki na kuhudhuria kwenu ndio mafanikio ya shughuli hii.
 
 
Mungu Ibariki Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania. Mungu ibariki Afrika. Amin.
 
Ahsanteni,
 
Katibu mteule Tanzaseattle.
 
Haji Rajab Haji.
 
.............

Kwa maoni au masuala munaweza kuwasiliana na:

Mwenyekiti: Emil Muta: 206 291 8835
Katibu: Haji Rajab Haji: 206 302 9404

No comments: