Advertisements

Tuesday, December 16, 2014

DIAMOND AVUNJA REKODI MAENEO MENGI

WIKI iliyopita katika simulizi hii ya Diamond tuliishia pale ambapo staa huyo aliongelea namna wimbo wake wa Mbagala ulivyopendwa kiasi cha kumfanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete ‘JK’ kumteua kuwa mburudishaji kwenye ziara za kampeni ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, mwaka 2010.Wiki hii tunaendelea

Oktoba 2, mwaka 2010, Diamond alipata safari yake ya kwanza kabisa ambapo alikwenda jijini London, Uingereza na kufanya shoo.Mwaka 2011, Diamond alishinda Tuzo ya

Nzumari iliyotolea nchini Kenya akiwa Msanii Bora wa Kiume toka Tanzania.
Diamond aliweka rekodi ya msanii wa kwanza Bongo kufanya shoo kwenye Ukumbi wa Maisha Club jijini Dar na kujaza mashabiki wengi kiasi kwamba wengine walishindwa kuingia ndani ya ukumbi huo.

AACHIA ALBAMU YA PILI
Ilikuwa Januari, 2012 Platnumz aliachia albamu yake ya pili na kufikia rekodi ya kuwa msanii nambari wani Bongo kuuza kopi zaidi ya 1,200,000.

Mwaka huohuo, Diamond alifanya shoo bab’kubwa iliyoitwa Diamonds are forever iliyofanyika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar kwa kiinglio cha shilingi 50,000. Diamond alikuwa peke yake na aliuza tiketi zaidi 1,500.

MSANII WA KWANZA BONGO KUSHUKA UWANJANI NA CHOPA
Mei, 2012, Diamond aliweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza kufanya shoo ya nguvu na kujaza zaidi ya watu 10,000 kwa kiingilio cha 20,000 ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live huku akishuka uwanjani hapo na chopa (helikopta). Hata hivyo, Desemba 25, mwaka huu (Krismasi), Diamond atakuwepo tena ndani ya Dar Live!

AENDA ULAYA, AKAMUA
Mwaka huohuo 2012, Diamond alifanya
ziara Ulaya ambapo alitembelea nchi kadhaa kama Italia, Uholanzi, Sweden na Ugiriki, nako alifanya shoo za nguvu.

Nyota ya 2012 ilizidi kuwa nzuri kwa Diamond kwani aliachia nyimbo mbili kwa mpigo, Nataka Kulewa na Kesho zilizoambata na video zake zenye ubora.

AWA BALOZI
Mwanzoni mwa mwaka 2013, Diamond alichaguliwa kuwa balozi wa kampuni moja ya vinywaji baridi nchini na kufanya ziara nchi za Afrika Mashariki, Burundi, DRC, Kenya, Uganda na Rwanda na kuwa msanii wa kwanza katika nchi za ukanda huo kupiga shoo peke yake kwenye uwanja na kujaza zaidi ya watu 30,000.

ASHINDA TUZO TENA
June 2013, Diamond alishinda tuzo mbili za Tanzania Kili Music Awards akiwa Msanii Bora wa Kiume wa Bongo Fleva na Msanii Bora wa Kiume kwa wanamuziki wote nchini.

NUMBER ONE
Julai 2013, Diamond aliachia singo ya Number One ambayo video yake aliifanyia jijini Capetown, Afrika Kusini na Kampuni ya Ogopa Video. Aliweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza kuzindua video hiyo bila kiingilio ndani ya Hotel ya Serena na kuwaalika viongozi mbalimbali.

Katika uzinduzi huo, Diamond alifanya tukio la kihistoria ambapo alimzawadia gari aina ya Totoya FunCargo aliyekuwa mwanamuziki nguli nchini, marehemu Muhidin Maalim Gurumo.

Itaendelea wiki ijayo.
GPL

No comments: