
Kwenye picha anayepandishwa kwenye kalandinga na mkimbiajia wa marathon Deogratiua Lazaro alipomvamia mkimbiaji mbio mwenzake Fabian Joseph na kmjeruhi kwa kumuuma mkono kwa tuhuma za uchawi kwenye mashindano ya mbio za Uhuru marathoni zilizokua sehemu ya sherehe ya miaka 53 ya Uhuru .
MBIO za Uhuru Marathon msimu wa pili zilizofanyika jana kwenye viwanja vya Leaders Club, kwa kiasi fulani zilitiwa dosari kutokana na baadhi ya wanariadha kushutumiana kwa mambo ya kishirikina.
Tukio hilo la aina lilitokea baada ya mkimbiaji Fabian Joseph kutoka Arusha kuvamiwa na mchezaji mwenzake, Deogratius Lazaro akimtuhumu kuwa ni mshirikina.
Katika hali isiyo ya kawaida, ilitokea baada ya kwisha kwa mbio za kilometa 21, ambapo Lazaro alimfuata na kumvamia Fabian akimweleza kuwa ni pepo huku akimshika mkono wa kushoto na kumng’ata dolegumba la mkono wa kushoto.
Asakari Polisi walikuwa wakilinda usalama wa mbio hizo, waliingilia kati kwa kumkamata Lazaro na kumpandisha katika gari yao na kuondoka naye katika eneo la tukio huku Fabian akikimbizwa katika Hospitali ya Mwananyamala.
Kwa mujibu wa mashuhuda, wanariadha hao walionekana muda mrefu wakizozana wakishutumiana juu ya masuala ya ushirikina hadi mwishowe kuishia kushikana.
Fabiani akizungumzia tukio hilo, alisema haelewi ni kwanini alivamiwa hadi kujeruhiwa kwa meno kwani wakati huo alikuwa akijiandaa kupumzika.
Alipotafutwa Mratibu wa mbio hizo, Innocent Melleck, alikiri kutokea kwa hali hiyo na kuongeza kuwa tukio jingine lilikuwa ni wanariadha wawili kutoka Kenya kuzuiwa kushiriki kutokana na kutokuwa na mwaliko rasmi.
Nje ya dosari hizo, mbio hizo zilifana ambapo Fabian alishinda kwa upande wa wanaume kilomita 21, hivyo kupata kitita cha shilingi mil 2.5; medali ya dhahabu na cheti. Mshindi wa pili katika mbio hizo, alikuwa ni Alfonce Felix wa klabu ya Holili ya Arusha akitumia saa 1:05.8, akipata sh mil 1 na Elia Daud (Arusha) akipata nafasi ya tatu na kupata sh 700,000.
Kwa wanawake ambao nao zawadi zao kwa mshindi wa kwanza hadi tatu zilikuwa kama wanawame; mshindi wa kwanza ni Catherine Range wa Arusha, Mary Naali na Furaha Sabaya kutoka Klabu ya Holili, Arusha.
Aidha, mshindi wa tano hadi 10 kwa wanaume na wanawake, kila mmoja alipata shilingi 100,000. Dosari nyingine katika mbio hizo, ilikuwa ni wanariadha kupotea njia.
Credit:Tanzania Daima
1 comment:
Angalia baadhi ya askari wanavyokuwa wanyama.Sasa huyo askari kumkanyaga na boot ni nini?Huyo ni mchezaji hata kama angekuwa mwizi mfano ,askari kazi yake ni kulinda raia.Lini itakuwa mwisho wa unyama huu wa askari wa kwetu huko?
Post a Comment