Waziri Mizengo Pinda amekatiza kwa muda, ziara yake katika Falme za Kiarabu kwa maelezo kwamba ameitwa nyumbani na Rais Jakaya Kikwete kwa shughuli maalumu.
Waziri Mkuu ambaye yuko katika ziara ya kutembelea nchi za Falme za Kiarabu, ikiwa ni sehemu ya kudumisha ushirikiano na kutafuta wawekezaji, amekatisha ziara hiyo siku mbili baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema kujiuzulu kutokana na kashfa ya Escrow.
Kwa mujibu wa ratiba ya ziara hiyo, leo Waziri Mkuu alitarajiwa kufanya mazungumzo na washiriki wa maonyesho ya B2B pamoja na kutembelea maeneo mengine lakini ziara hiyo imefutwa na badala yake anaondoka asubuhi kurudi nyumbani.Baadaye leo Pinda alitakiwa kwenda Doha, Qatar kwa ziara kama hiyo hadi Desemba 23.
Baada ya kukamilisha jukumu aliloitiwa, Waziri Mkuu anatarajiwa kurejea Falme za Kiarabu Jumamosi kuendelea na ziara yake.-BBC
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii nchini, Devota Mdachi (kushoto) na Mwenyekiti wa Kampuni ya Nakheel PSSC ya Dubai, Bw, Ali Lootan wakizungumza katika Mkutano wa Kuitangaza Tanzania na kuvutia wawekezaji wa Dubai uliofunguliwa na Waziri Mkuu mjini Dubai Desemba 17, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongozwa na Meneja Mkuu wa Shamba la kufuga ng'ombe wa maziwa la Al Rawabi Dairy la Dubai, Dr. Ahmed Al Mansour (kulia kwake) kukagua shamba hilo akiwa katika ziara ya kikazi nhini humo Desemba 17, 2014
Waziri Mkuuu, Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa Meneja mkuu wa shamba la kufuga ng'ombe wa maziwa la Al Rawabi Dairy la Dubai, Dr. Ahmed Al Mansour (kulia) wakati alipotembelea shmaba hilo akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo Desemba 17, 2014.
No comments:
Post a Comment