Advertisements

Monday, December 22, 2014

KIKWETE AHUTUBIA WAZEE LEO JIJINI DAR ES SALAAM


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh.Saidi Mecki Sadiki akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuzungumza na Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo alimpa taarifa Mheshimiwa Rais juu ya mafanikio ya ujenzi wa maabara katika Shule za Sekondari mjini Dar es Salaam pamoja na matokeo ya uchaguzi wa Serikali za mitaa.(Picha na Adam Mzee)

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam ambao waliitika wito wa kumsikiliza wakati wa kulihutubia Taifa kupitia Wazee kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam.( Picha na Adam Mzee
 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisoma hotuba yake kwa Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. ( Picha na Adam Mzee)
 Baadhi ya Wanasiasa wakongwe waliohudhuria.
 Kila wilaya ya mkoa wa Dar es salaam iliandaliwa sehemu maalum ya kukaa.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia Taifa kupitia Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo alizungumzia uchaguzi na kutaka polisi kufanya kazi yao katika kuhakikisha uchaguzi ujao uchaguzi hauvurugwi na pia alifafanua mambo mbali mbali yaliyokuwa yakizungumziwa kuhusu akaunti ya ESCROW na kumwajibisha Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka.
 Ukumbi wa Diamond Jubilee ukiwa umefurika Wazee waliokuja kumsikiliza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.
 Ukumbi ulifurika kila kona.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo wakati wa ufafanuzi wa masula kadhaa yaliyoleta mkanganyiko kwenye sakata la Escrow Akaunti.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya mrisho Kikwete akipanga makaratasi yenye hotuba yake wakati wa kuhutubia Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam.

Wananchi wakishangilia baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhitimisha hotuba yake kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar Es Salaam.

10 comments:

Anonymous said...

I feel sorry for this Professor, she should have resigned long time ago, now she has been sacked and likely to be charged and sent to a gereza. From UN to Ukongo or Keko, hapo siipati. This should be a lesson to all Professors and Drs who enter politics. We have so many of them and yet no good policies. All we hear everyday is ufisadi at the highest level...

Anonymous said...

Msomi lakini hakuelimika. It's quite embarrassing kusikia professor akitoa utetezi kama aliokuwa anautoa huyo mama! She knows or should know that a government leader anywhere in the world should never be a player in any business or nongovernmental entities, to avoid conflict or the appearance of conflict of interest. I wish Tanzania ingekuwa serious na kutoa fundisho kwa viongozi uchwara kama hawa.

Anonymous said...

Mheshimiwa raisibkwanza tunashukuru kwa kulifanyia kazi hilo...mbili. .naomba niulize kwa hawavwatu kila siku wanajiuzuru au wanasimamishwavhalafu ndio nini.? Bungeni upo serikali inamlipa kazi kasimamishwa..ndo biashara kwisha.wizi wizi ..jamani haitoshi Tibaijuka awajibishwe nabjela aende iwe mfano..asituambie story zake kwamba alipewa pesa ziende account yake ni masharti aliopewa na mtoaji? Mtoaji nani? Nae aende ukonga/segerea hii tabia iishe ya wizi..miaka nenda mbele nyuma tunaibiana , Lowasa kaiba kaka kimya imeisha na anakula pesa yake mpaka sasa hamna yeyote anemwamvia chochote. .wahusika wawajibishwe na wasifanye tena kazi za umma..ni watu wasiojali masilahibya wananchi wa kawaida..raisi kikwete tunataka majibu yab haraka tumechoka dana danaza kienyeji

Anonymous said...

Uongozi huu wa JK ni wa aina yake sana. Ni uongozi wa kihistoria sana hasa kwa mantiki mbili kuu za msingi ambazo zimelifanya taifa au watanzania kuwa maskini sana. 1. Ni uongozi unaoongoza sana kwa wizi wa mali ya umma kwa sababu ni wa kizazi cha wasomi sana. 2. Ni uongozi unaolindana sana ingawa wachache wao tu ndio hulazimika kujiuzulu. Nao hujiuuzulu sababu wamechuma sana mali. Kwa mfano sasa hivi wako katika lala salama ya kumaliza uongozi wa awamu yao hivyo kila mtu anabeba chake na kila kiongozi anajivunia kwa kuteiliwa na JK ktk awamu zote sababu wanatoka wakiwa wanono wao na familia zao. DHAMBI KUBWA SANA HII. JK hana hofu yote haya sababu ni baba wa haya
Haiwezekani aseme eti bodi ya TANESCO muda wake umekwisha, na General Atorney nae kamaliza kwa kujiuzuru...... haitoshi hii kabisa. Hata kama kajiuzuru sawa, sababu kujiuzuru ni sehemu ya kuwajibika bado adhabu iko pale pale. kuhukumiwa na kufilisiwa mali zote. Tibaijuka sikomenti chochote sababu ni roten egg.

Anonymous said...

hakuna kitu movie inaendelea tu sijui ziko part ngapi, mtakuja kuniambia ni kamchezo tu haka tukiwa hai tutakuja kuwaona wapo tena serikalini hakuna kuwajibishwa wala nini.watalipwa pesa zao kama wako kibaruani.ni upepo tu unapita wache upita chezea ccm weweee

mnadanganywa nyinyi wadanganyika.

Anonymous said...

mpwa tuweke basi ka clip cha video tuwaone na kuwasikia au hata ka clip cha audio tuwasikiye please mpwaa.ahsante

Anonymous said...

Nasema sisi Watanzani ni mijitu mijinga mijinga kama kijinga cha moto, tunapigia kelele tuu kwa vijisenti twa escrow, ambayo sio chanzo ni matokeo tuu!.

malipo hayo ya IPTL yanayobishaniwa ni kiwango cha capacity charges tuu, mkumbuke IPTL bado inameza mabilioni kadhaa ya utility kila siku iendayo kwa Mungu!, nobody cares!.

Turudi kwenye mgao wa Escrow, PAP amegawa 'sadaka' kubwa kubwa nene nene, kwa 'wanene' kupitia Stabic Bank, kwa vile majina hayajatajwa, then its ok!. JR amegawa sadaka kubwa kubwa nene nene, kwa 'wanene' kupitia account yake iliyoko Uholanzi, majina yapo na viwango vipo, na wanajulikana!, ila kwa vile hawajatajwa,sisi Watanzania mazuzu tunashangilia Tibaijuka amewajibishwa!.

Nahisi sio wengi wanaojua kuwa IPTL/PAP bado inaidai Tanesco nyingi kuliko fedha zote zilizokuwemo escrow!, na kwa vile bado IPTL inazalisha umeme, deni hilo linaongezeka siku hadi siku, na malipo yake yatafanyika direct kutoka Tanesco into IPTL/PAP kimya kimya!, and life goes on!, nobody cares!, watu wanashangilia ujinga kwa kuangalia tulipoangukia baada ya kujikwaa, badala ya kuangalia tulipojikwaa!.

SO SAD,GOD HELP US TANZANIANS.

Anonymous said...

Leo Prof. Tibaijuka amewajibishwa, wengi kuanzia ukumbini kule hadi humu vijimamboni wanashangilia!, wanashangilia nini?, wanashangilia ujinga?!.

Ukweli nchungu ni uamuzi huo ni muendelezo wa ile ignoran, hivyo wale mnaoshangilia kuwajibishwa kwa Prof. Tibaijuka, mnashangilia ujinga!. Tibaijuka amewajibishwa kwa kosa gani?!.

Nasema wale mnaoshangilia, nimesema mnashangilia ujinga kwa sababu kosa la Tibaijuka sio kupokea pesa, bali kujulikana kuwa amepokea pesa!. Majina yaliyotolewa ni kwa waliopokea pesa kupitia Benki ya Mkombozi tuu, vipi waliopokea pesa za PAP kupitia Stanbic?!, hawana makosa simply kwa sababu hawakutajwa?!. Vipi waliolipwa na JR kupitia account yake ya Holland?. What a double standard?!.

Ila pamoja na kumfanya Tibaijuka ndiye kondoo wa kafara, ili tuu serikali iwafurahishe wafadhili kuwa we are doing something, unless hao wafadhili nao they are fools!, ndio wataukubali ujinga huu!.

Anonymous said...

Of all the people sio member wa JF wanaoonekana kuwa na upevu walau kidogo kushindwa kuchambua issues.

Kuna mambo mengi ya kutia shaka....watu hatuhoji

Kikubwa tulichoona ni tweets za mtoto wa Tibaijuka

Kwa nini kikwete anasimamia maslahi ya IPTL badala ya TANESCO ...Watu hatujiulizi

Kwa nini ameongea kwa kubeza sana kwamba pesa zimebebwa kwa magunia

Kwa nini ame ignore ishu za stanbic

Nini kitafanyika kuhusu Mkataba wa IPTL ,,,Bado kimya

Halafu mapoyoyo ya vijimambo yanashangilia Tiba kuondolewa just because yeye amejulikana kachukua pesa

Nani waliochukua mapesa mengine...thats non of our business

Najuta kuwa mtanzania...deep from my heart

Anonymous said...

Ni hakika hatuwezi kuzungumzia IPTL bila kuwagusia WOTE walopata kalia kiti cha waziri anayehusika na Maji, Nishati, Madini.....Kuanzia 1993 mpaka leo......