Advertisements

Monday, December 22, 2014

Maalim Seif kumvaa Dk Shein kuhusu ukaazi

Zanzibar. Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema atapambana katika vikao na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein iwapo baadhi ya wananchi wataendelea kunyimwa shahada za wapigakura kwa kisingizio cha ukaazi.
Maalim Seif alitoa msimamo huo jana alipohutubia mkutano wa hadhara wa CUF uliohudhuriwa pia na Mwenyekiti wake, Profesa Ibrahim Lipumba katika Uwanja wa Jarida, Wete Pemba.
Alisema kuna viongozi wa Serikali za Mitaa (masheha) kwa kushirikiana na wakuu wa wilaya na mikoa ambao wameanza kupanga mikakati ya kutaka kuwanyima shahada za wapigakura baadhi ya wananchi kwa madhumuni ya kuibeba CCM katika uchaguzi mkuu.
“Masheha eleweni nazungumza kama makamu wa kwanza wa rais, suala la ukiritimba sasa basi na kama hamtaki sisi tutapambana na Dk Shein katika vikao yeye, ndiye anayewateua,” alisema Maalim Seif.
Kwa miaka mingi yamekuwapo malalamiko kutoka CUF kwamba masheha wamekuwa wakiwanyima vitambulisho vya upigaji kura baadhi ya Wazanzibari, wakisema si wakaazi wa Zanzibar.
Akishangiliwa na wafuasi wa CUF, Maalim Seif alisema kama mipango itakwenda kama ilivyopangwa, hakuna wa kuizuia CUF kuingia Ikulu, hivyo akawataka wana-CUF kuendeleza umoja na mshikamano kabla ya uchaguzi huo.
Alisema umoja ni nguvu na ndiyo maana Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), umefanikiwa kuandika historia mpya katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa baada ya kupata matokeo ya kuridhisha.
Mwanasiasa huyo alisema madhara ya kukataa umoja ndiyo yaliyoiathiri Zanzibar katika Bunge la Katiba baada ya wajumbe wake kutetea masilahi ya chama badala ya nchi.
Akihutubia mkutano huo, waziri wa zamani wa SMZ, Mansoor Yusuph Himid alisema njia ya Maalim Seif kuingia Ikulu mwakani ni nyeupe.
Alisema CUF kipo imara na kwamba jambo muhimu ni wanachama na wafuasi wake kuendeleza umoja na mshikamano kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo.
“Njia ya kuingia Ikulu nyeupe, muhimu tukaze buti kufikia malengo ya kuleta mabadiliko ya kweli,” alisema Mansoor.
Profesa Lipumba alisema suala la Katiba ndiyo limeimaliza CCM katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kutokana na wananchi wengi kupinga kitendo cha rasimu ya Jaji Warioba kubadilishwa na kuondoa vifungu muhimu vilivyokuwa vikiwabana mafisadi na viongozi wasiokuwa waadilifu.
“Matokeo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa yameonyesha dalili kuwa CCM ipo katika hatari ya kufa na kukifuata chama cha Kanu cha Kenya,” alisema Lipumba.
Alisema Serikali imeshindwa kusimamia utawala wa sheria na ndiyo maana watuhumiwa wa wizi wa Sh306 bilioni katika Akaunti ya Tegeta Escrow wameendelea kutamba bila ya kuchukuliwa hatua.
Alisema Bunge lilipitisha maazimio la kutaka watuhumiwa hao wafukuzwe katika nyadhifa zao na kuchukuliwa hatua za kisheria lakini hadi sasa hakuna utekelezaji, wameendelea kubakia katika ofisi za umma licha ya kukabiliwa na kashfa nzito.
Alisema kutokana na kushindwa kusimamia utawala wa sheria, ndiyo maana hata watuhumiwa katika kashfa ya Akaunti ya Madeni ya Nje (Epa) hawakuchukuliwa hatua za kisheria na badala yake kutakiwa kurejesha fedha.
Mwananchi

2 comments:

Anonymous said...


Tunauthamini mchango wako Maali na cuf sana kwa kutetea haki za wanzibari, cha msingi ni kuweka mikakati imara juu ya kuhakikisha kila mtu anaandikishwa na tume ya uchaguzi inavunjwa kwanza. na jinsi ya kupanga mikakati sio kuongea na raisi wa kum’bana raisi taasisi ya uraisi zanzibar ni ukaragosi tu hamna kitu, nchi na raisi wake wanaendeshwa kwa remote tu,


ccm hata sikumoja hawato fanya jambo kwa faida ya cuf. Labda kwa bahati mbaya. Kwa hivyo Maalim lazima muwe na mikakati yanu madhubuti. Kwani ccm wa Zanzibar wame ekwa hapo kuvuruga maedeleleo ya Wazanzibari ki jamii na kisisasa. Ili iwe koloni la Tanganyika milele.

.Ikiwa Mbunge,Mwakilishi na Diwani wa mji mkongwe au Wete ni CUF kwa nini Sheha wa shehia awe wa CCM wakati ni jimbo la CUF kwasababu ikiwa ni Sheha atakuwa ni wa CUF basi wafuasi wote wa CUF wataandikishwa bila ya malalamiko yeyote yale kwani kila unachokitaka kukipata ni lazima uwende kwa Sheha sio Diwani,Mwakilishi wala Mbunge.Kwahio ushauri wangu kwanza tuwaondowe hawa Sheha kwenye majimbo yetu ikisha tutakwenda kutatua jengine. Bila ya hilo CUF watalalama mpaka CCM ife Tanganyika.

Anonymous said...

Vyumba va kupigiya kura .sisemi visanduku .vyumba va kupigiya kura viangaliwe zaidi kuna tetesi kuwa kwenye floo au sakafu huwa wanachimba kama kihandaki na kuna visanduku kama hivo mlokwiisha kuvipigiya kura .huwa wanavibadilisha bio mbio bila watu kujuwa . SIJUWI KAMA KWELI AU UWONGO .MAANA Hii mi CCM inaweza.