Monday, December 8, 2014

MAMA BISHANGA AMPONGEZA DIAMOND

Nimeona nisikae na duku duku la pongezi zangu kwa kijana wetu Diamond kwa kutwaa tunzo tatu kwa mpigo wiki iliopitai huko South Africa, huo ni ushindi mkubwa sana kwa Diamond, na sisi sote kama taifa la Tanzania. Mimi kwa niaba ya wazazi wenzangu bwana mdogo nakupongeza sana na ninampongeza sana mama yako Sandra kwa kukuandaa katika fani ya muziki, nguvu yake ndio mafanikio yako. 

Hii inanikumbusha hata mimi nilivyokuwa ninaandaa kazi zangu za sanaa wakati nafundisha Chuo cha Uhazili Tabora nilimtumia mwanangu Kenny (Hery) kuigiza nae na kucheza nae ili kumuelekeza mkondo uigizaji. Na hata Natasha alifanya hivyo kwa mwanae Monalisa, na wengineo wengi, kumbe ni jambo zuri kwa wazazi kufanya hivyo kwa watoto wao kwa fani mbalimbali, ili kuwapa msingi bora wa kazi zao katika maisha yao.

Mimi ninakukubali sana kimuziki na kimaadili na upendo na heshima unayompa mama yako na jamii nzima. Na hii ngololo, ngololo, ngoololooo hii kiboko hata sisi wazazi wako hii tunaisakata kama kazi! kama unavyoona hata jikoni ngololo inakubali sana, halafu inafanana kidogo na ngoma ya kwetu ya wayao inaitwa nsobe, hiyo nayo huchezwa zaidi na vijana.

Keep up young boy from Tanzania! Home , sweet home Tanzania.

Mama Bishanga/ Mrs Marolen
Ohio/ USA

No comments: