Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Kamilius Membe (Mb.) ameagana na Balozi wa Australia nchini Tanzania Mhe Geoffrey Tooth ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi nchini.
Waziri Membe akizungumza na Balozi Tooth na kumweleza kuwa wakati wa kipindi chake cha uwakilishi, uhusiano baina ya nchi hizi mbili umeimarika. Mhe. Membe pia amemshukuru Balozi Tooth kwa ushirikiano mzuri alioutoa katika kipindi chote na kusisitiza kuwa Tanzania ni nyumbani kwake sasa na asisite kurudi nchini kutembea au kwa mapumziko mara apatapo fursa ya kufanya hivyo.
Mazungumzo yakiendelea kushoto wa kwanza ni Katibu wa Tatu wa Ubalozi huo Bi. Freya Carlton.
Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki akizungumza na Balozi wa Australia ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini.Picha na Reginald Philip
No comments:
Post a Comment