ANGALIA LIVE NEWS

Friday, December 12, 2014

MWIGULU NCHEMBA ALIPOPITA HII LEO ITILIMA MKOANI SIMIYU KUWAOMBEA KURA WAGOMBEA WA CCM


Mh:Mwigulu Nchemba akichambua kuhusu swala la Uadilifu wa Viongozi na Watumishi wa serikali,Kuna
watumishi wa serikali ambao hawana Vyama au sio wanaCCM lakini Wanaiba Serikalini  na dhambi hiyo inakwenda CCM.Hivyo ni muda muafaka wa Kutenganisha Wezi,mafisadi na CCM.Comrade Mwigulu Nchemba akinadi na kuwaombea kura wagombea wa ngazi zote wa CCM kata ya itilima mkoani Simiyu.Comrade Mwigulu Nchemba akisalimiana na Wananchi wa Itilima hii leo.Mwigulu Nchemba akiwaeleza wanaitilima Mkoani simiyu hii leo kuwa CCM ndio chama chenye Ilani inayotekelezwa,Hivyo wananchi wachague viongozi wa chama cha mapinduzi wanaojua Ilani inasemaje juu ya Wanaitilima.Mwigulu Nchemba akiagana na Wananchi wa Itilima mapema Mchana wa leo baada ya kumalizika kwa Mkutano wa kuhamasisha wananchi kujitokeza kupiga Kura hapo kesho kutwa kwenye Uchaguzi wa serikali za Mitaa.

No comments: