Baadhi ya watu waliojeruhiwa katika uvamizi uliofanywa na raia wa Iran na kuwateka nyara watu ndani ya mgahawa
Uvamizi ambao umeendelea kwa masaa 16 nchini Australia ambapo mwanamume aliyekuwa amejihami na kuwateka nyara watu ndani ya mgahawa mmoja mjini Sydney umemalizika.
Mvamizi huyo anasemekana kuwa raia wa Iran kwa jina Haron Monis.
Katika matukio ambayo yameonyeshwa moja kwa moja kupitia televisheni, polisi walifyatua risasi huku milio mikubwa ya risasi ikisikika huku baadhi ya mateka wakikimbilia usalama wao.Bwana Moni anajulikana sana na polisi kwa rekodi yake ya uhalifu
Baadhi ya watu waliojeruhiwa kufutia ufyatuaji huo wa risasi walipelekewa hospitalini. Inaarifiwa watu kadhaa wamejeruhiwa. Hali ya mvamizi huyo anayesemekana kuwa na umri wa miaka 49 bado haijajulikana.
Mwanamume huyo alikua ameachiliwa kwa dhamana kwa makosa mbali mbali aliyokuwa ameshitakiwa nayo. Moja ya makosa yake ilikuwa kuwatumia barua ya matusi wazazi wa wanajeshi wa Australia waliofariki wakiwa wanatumikia jeshi la taifa hilo nchini Iraq.
Waziri mkuu Tony Abbott alisema lilikuwa jambo la kushtua sana kwamba wananchi waiso na hatia walitekwa nyara na mtu ambaye alikuwa anashinikizwa kisiasa.
Makomando wa jeshi walifyatua risasi na kisha kuingia ndani ya mgahawa huo huku wakirusha magurunedi. Inaarifiwa watu wengi walijeruhiwa
MTU mmoja mwenye silaha bado anaendelea kuwashikilia wafanyakazi na wateja katika mgahawa wa Lindt uliopo jijini Sydney nchini Australia.
Watu watano wameonekana wakikimbia kutoka katika jengo hilo la mgahawa japo mpaka sasa bado haijafahamika ni mateka wangapi wapo ndani.
Askari polisi waliozingira eneo lote la mgahawa huo wameeleza kuwa tayari wameanza kufanya mazungumzo na mtekaji huyo aliye ndani ya jengo.
Mateka ndani ya mgahawa huo wakiwa wameshika bendera yenye maandishi ya Kiarabu.
Baadhi ya watu ndani ya jengo hilo wameonekana kupitia madirisha wakiwa wamebeba bendera nyeusi zenye maneno ya Kiarabu.
Ulinzi mkali nje ya mgahawa.
Watu watano wameonekana wakikimbia kutoka katika jengo hilo la mgahawa japo mpaka sasa bado haijafahamika ni mateka wangapi wapo ndani.
Askari polisi waliozingira eneo lote la mgahawa huo wameeleza kuwa tayari wameanza kufanya mazungumzo na mtekaji huyo aliye ndani ya jengo.
Baadhi ya mitaa ikiwa imefungwa.
Mpaka sasa bado haijafahamika sababu za mtu huyo kuwateka watu ndani ya mgahawa huo.-.-BBC
No comments:
Post a Comment