Kama ambavyo iliwahi kutamkwa huko nyuma, historia ya Mengi inamuonyesha kwamba ni mtu anayependa kuanzisha ugomvi katika mambo yanayohusu maslahi yake binafsi lakini unapopamba moto na kuona anazidiwa, hutafuta hifadhi kwa kulia lia na kutaka aonewe huruma na kutaka kuliingiza Taifa zima. Katika kufanikisha hayo, amekuwa akitumia vyombo vyake vya habari kuwapotosha wananchi ili waone anaonewa au eti anapigania maslahi yao. Hiii ina jidhihirisha wazi kutokana na mlolongo wa ugomvi aliowahi kuuanzisha dhidi ya watu mbali mbali kwa sababu anazozijua yeye mwenyewe.
a) Alianzisha ugomvi na wamiliki wa vituo vya televisheni vya DTV na CTN mwaka 1994 kwa hofu tu ya kwamba watakuwa washindani wa kituo chake cha ITV na akafika hatua ya kuwazushia kwamba wanataka kumuua, akaufanya ni ugomvi wa nchi nzima.
b) Alianzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Utawala Bora, Mheshimiwa Wilson Masilingi, baada ya kushindwa zabuni ya ubinafsishaji wa Hoteli ya Kilimanjaro, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima. Katika kudhihirisha jinsi alivyo mtu wa chuki na visasi, kutokana na kuikosa tu hoteli hiyo, amekuwa hakanyagi na hata hashiriki shughuli yoyote inayofanyika katika hoteli hiyo.
c) Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda, Mheshimiwa Shamim Khan, kwa kutakiwa afute maelezo katika maji ya kunywa yanayozalishwa na kampuni yake kwamba yalikuwa ya chemchem wakati hayakuwa hivyo, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.
d) Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Mazingira, Mheshimiwa Edward Lowassa, aliyemkanya Mengi asitumie nafasi yake kama Mwenyekiti wa Baraza la Mazingira kuwakomoa washindani wake wa biashara kwa kuwazushia tuhuma za kuchafua mazingira na kuvifungia viwanda vyao, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.
e) Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Basil Mramba, baada ya kumnasa akikwepa kodi katika uendeshaji wa biashara yake ya bahati nasibu ya BINGO, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.
f) Akaanzisha ugomvi na kampuni ya Habari Corporation iliyokuwa inaongozwa na Jenerali Ulimwengu baada ya kufichua habari za jinsi alivyoifilisi benki ya NBC, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.
g) Akaanzisha ugomvi na mfanyabishara Yusuf Manji ambaye kwanza walikuwa wakigombea uendeshaji wa mchezo wa bahati nasibu, na baadaye akajenga chuki naye binafsi kwa sababu tu alifanikiwa kuusuluhisha mgogoro wa Yanga ambao Mengi ulimshinda, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.
h) Akaanzisha ugomvi na Mheshimiwa Adam Malima ambaye alihoji Bungeni jinsi Mengi anavyotumia vibaya vyombo vyake vya habari kwa kutangaza habari za kujitukuza binafsi zaidi ya hata vinavyotangaza habari zinazowahusu viongozi wa kitaifa, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.
i) Akaanzisha ugomvi na mfanyabiashara Tanil Somaiya baada ya kumuona kijana huyo aliyekuwa wakala wa kuuza bidhaa za viwanda vyake Mengi (kabla ya kuviua mwenyewe), ameweza kujiimarisha na kupata mafanikio makubwa ya kibiashara hata kumshinda yeye Mengi, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.
j) Akaanzisha ugomvi na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Lawrence Masha, kwa kuja na madai ya kutaka kuhujumiwa, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.
k) Akaanzisha ugomvi na Ndugu Rostam Azizi, baada ya kuona kwamba amekuwa mshindani wake mkubwa katika umiliki wa vyombo vya habari hapa nchini, na aka ufanya ni ugomvi wa wa nchi nzima.
l) Akaanzisha ugomvi na vijana wajasiliamali wa kikundi cha Zecomedy kisa baada ya wao kugundua ana wanyonya kwenye maslahi yao kupitia mkataba wa kipuuzi aliokuwa nao dhidi yao hali iliyo pelekea wao kuvunja mkataba na kujiunga na TBC.
m) Akaanzisha ugomvi na Waziri wa Sayansi na Teknolojia Prof. Mbarawa Makame baada ya serikali kupitisha azimio la kubadili mfumo wa matangazo kutoka analojia kwenda digitali ambapo alikuwa akishinikiza watanzania wakatae kwa lengo la yeye mwenyewe kujinufaisha binafsi.
n) Ni huyu huyu Reginald Mengi amekuwa akipiga vita ya chini kwa chini kuhakikisha Tanzania haipati katiba bora kwa malengo yake binafsi na huu ni mpango mkakati anao uratibu kwa kushirikiana na UKAWA na baadhi ya balozi za kutoka nchi ya wahisani ambazo haziitakii mema nchi yetu.
o) Baada ya kuona malengo yake pamoja nay a UKAWA hayatimii akaanzisha kampeni ya hadharani kuhakikisha bunge hilo lina simama mara moja kabla ya muda wake. Hali hii ilipelekea kukemewa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge hilo maalumu Mhe Samweli Sita ambapo sasa kaanzisha ugomvi binafsi na waziri husika kwa kuhakikisha hapati nafasi kwenye vyombo vyake vya habari.
p) Na kama hiyo haitoshi, akamfadhili Ndugu Said kubenea akafungue kesi mahakamani ili kusimamisha Bunge maalumu la katiba. Na bado penyewe wakashindwa.
q) Baada ya kugaragazwa mahakamani sasa amegeuka kuwa mfadhili mkuu wa NYERERE Foundation ambayo inatumiwa kama kivuli cha kuhakikisha waliokuwa wajumbe wa tume ya katiba wana ipinga hadharani katiba pendekezwa.
r) Na siku za karibuni kaanzisha ugomvi mkali na Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospter Muhongo baada ya kuona harakati zake za kutaka kupewa vitalu vya gesi bure kwa kigezo cha uzawa kugonga mwamba. Amesikika mara zote akitoa maelekezo maalumu kwa wahariri wa vyombo vyake vya habari kuhakikisha wana mwandika vibaya Prof. Muhongo mpaka ang’oke wizarani.
HITIMISHO:
Watanzania tuna haja na kila sababu ya kujiuliza mara mbili mbili juu ya uhalali wa mtu huyu kuamua kutumia kigezo cha utetezi wa wanyonge (uzawa) kwa minajili ya kujinufaisha yeye binafsi, familia yake pamoja na washirika wake. Ni vyema pia tuendele kujiuliza uwapi uhuru wa vyombo vya habari kama wamiliki wa vyombo vya habari wanashinikiza kuandikwa habari wanazozitaka wao hali inayo tunyima fursa watanzania haki ya kupata habari kwa usawa. Ni vyema pia tujiulize uwapi uhalali wa mmiliki huyu anayejifanya ni mzalendo ilihali ana wanyanyasa wafanyakazi wake kwa kutowapa maslahi yao kama wanavyostahili. Sasa umefika wakati watanzania tuseme hapana. Kamwe hatuwezi kukubali hili na tunatoa wito kwa serikali kuchukua hatua kali dhidi ya mmiliki huyu ambaye amekuwa akichochea vurugu na kuivuruga serikali pasipo sababu. Pia tunatoa wito kwa watanzania kupuuza ujinga na upuuzi unaofanywa na mmiliki huyu katika kuhakikisha nchi hii inakosa amani kwa maslahi yake pamoja na genge lake la wahuni.
Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.
Mkishimundu
8 comments:
Mtoa hoja, you really drove this point home and made my day! Huu ndio ukweli wa mambo ambao siku zote nimekuwa nikitamani wanyonge, ambao tumekuwa tukitumiwa bila kujua kutia nguvu harakati za Mengi za kutetea maslahi yake binafsi, tuujue!
Muulizeni Mzee Mkapa alipokataa Mengi kuuziwa iliyokuwa Kilimanjaro Hotel wakati Mengi alikuwa na mpango wa mara tu ya kuinunua naye pia kuiuza na alikuwa ameshapata mnunuzi. Mzee Mkapa akamstukia. Chuki mpaka kesho.
Hadi leo Mengi hajawahi kuingia Kilimanjaro Kempiski. Ukweli asingeweza kuifanya kama ilivyo leo. Lengo lake ilikuwa kuipiga rangi na kuuza apate chake na kwenda. Lakini chuki ikawa yote kwa Serikali ya awamu ya Tatu na hiyo hoteli hadi kesho.
Hayo ya Muhongo mbona madogo! Mbinafsi sana Mzee huyo.
Mimi pia nilikuwa naona kuna kitu hapa, asante kwa kutufungua macho. He is too good to be true kwa kweli. Huyu aliwahi pia kuwa na mgogoro na waislam kipindi flani, sikumbuki vizuri...
Mengi mjanja sana. Mimi nilishamshtukia siku nyingi tokea mambo yake yakuchota mikopo NBC na kukataa kulipa
Acha udini wewe, hakuna ugomvi na waislaam. Mna matatizo sana ninyi mnaoleta mambo ya udini kwenye kila kitu, aligombana na waislaam wakiwa wapi? Ina maana mtu binafsi akikosana na sheikh mmoja amekosana na waislaam wote.....ebu mjifunze kufikiri, panueni elimu yenu na uwezo wa kufikiri siyo kufuata mkumbo tu. Ina maana Mengi au Bakhresa akikosana na padri au askofu anakuwa amekosana na wakristo wote? Acha akili na mawazo ya Boko Haramu,kwanza kama hukumbuki vizuri au hujui kwanini unaongea?
mtoa mada wa mwisho wewe unaonyesha udini, ilikuwa uijuwe story yote kwanza, halafu ucomment, kwa mfano nikitakaka kuchukua shamba la kijiji, huo ni ugomvi na wana kijiji, hapa hatujui ni ugomvi gani ulikuwa na waislam, alieandika ni mmoja wewe umewachanganya wote, kama ulikuwa wa kufikiri usingekuwa na mawazo pumba kama ulivyo, kumbe wewe ndie unahitaji kufikiri na kupambanua akili yako
Hii nayo ni siassa.
MNAJUA CHANZO CHA BOKO HARAMU msije na akili za kunywa mbege hapa fatiliyeni vikundi vyote hivi vya alkaeeda Boko haramu etc na mje hapa muwatusi watu na vijineno vyenu vya kuswambia waache akili na mawazo ya boko haramu.
acha kuvuta bangi za wajamaica wewe.
Post a Comment