ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, December 25, 2014

SALAMU ZA KRISMASI NA KHERI YA MWAKA MPYA KUTOKA UONGOZI WA JUMUIYA YA WATANZANIA NEW YORK

Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania New York,New Jersey,Connecticut na Pennsylvania unawatakia sikukuu njema wanajumuiya wote wa New York Tanzanian Community(NYTC).Tunakutakieni furaha katika sikukuu hizi,mapenzi pamoja na Afya njema,ni matumaini yetu kuwa mwaka tunaouaga ulikuwa ni mwaka wa kheri,mafanikio na baraka nyingi na kwa pamoja tunamuomba Mola aujaalie mwaka ujao 2015 uwe wenye mafanikio,Afya njema na adumishe umoja wetu ili tuendelee kushirikiana kama ambavyo tumeweza kufanya hivyo katika kipindi chote cha uhai wa Jumuiya yetu ya NYTC.

Uongozi pia unachukua fursa nyengine kukushukuruni kwa ushirikiano wenu mliouonyesha kwetu katika kuisimamisha Jumuiya yenu na kuhakikisha inasonga mbele.Tumezikabili challenge kwa pamoja na tutaendelea kufanya hivyo kwa manufaa ya umoja na udugu wetu kama ambavyo Watanzania tumezoeleka ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu.Hatutaziruhusu Dini,Kabila,Ubinafsi,ego au upuuzi wa aina yoyote kutugawanya ama kututenga na jumuiya yetu,Uimara wa Jumuiya yetu utajengwa na mbiu ya Utanzania wetu kwa manufaa ya wote.Shukurani tena kwa Hilo.

Shukurani nyengine za kumaliza mwaka kwa Mabalozi wetu wa kudumu umoja wa mataifa,Waheshimiwa Balozi Tuvako Manongi na Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi kwa ushirikiano wao wanaoendelea kutupa kuhakikisha Jumuiya yetu inaimarika.Mbali na kuwa wanachama wa Jumuiya yetu lakini pia kukubali kwao kuwa walezi wa Jumuiya yetu kwa kipindi chote tokea walipochukua mamlaka katika Balozi zetu Umoja wa Mataifa.Ulezi wao ni wa khiari pamoja na kazi zao nyingi za kiserikali,Uongozi unaheshimu sana ushiriki wao katika Jumuiya yetu.Shukurani nyingi pia kwa maafisa wote wa Ubalozi NY.Tunakutakieni sikukuu njema na kheri za mwaka mpya 2015.

Shukurani nyengine za kipekee kwa Mama Balozi wa Tanzania Marekani,Mama Liberata Mulamula kwa ushirikiano wake na Jumuiya yetu,Ushauri wake kwetu,juhudi zake za kuhakikisha tunaendeleza umoja wetu,Msimamo wake wa kuhakikisha Diaspora Marekani tunaimarika ili tuweze kuleta tija nyumbani Tanzania kama ambavyo Diaspora za nchi nyengine zilivyofanikiwa.Shukurani nyingi kwa maafisa wote wa Ubalozi Washington DC,sikukuu njema na kheri ya mwaka mpya 2015.

Muhimu:Taarifa hii itafuatiwa na attachment ya ripoti fupi ya fedha kutoka kwa waweka hazina wetu.

Kwa niaba ya Uongozi:Mkt.msaidizi Michael Chiume,Katibu Deo Mhella,Katibu Msaidizi Dr.Miriam Abu,Mweka Hazina Raphael Faida na Mweka Hazina Msaidizi Dr.Temba.

TUNAWATAKIA WATANZANIA WOTE SIKUKUU NJEMA NA KHERI YA MWAKA MPYA 2015

Hajji Khamis
Mwenyekiti
Jumuiya YA Watanzania New York.

8 comments:

Anonymous said...

Hivi kuna haja ya maneno yote haya kutoa Heri ya Xmas?

Anonymous said...

Hawa ndio wale shuleni walikuwa wanaamini kwamba wakijaza kurasa nyingi katika kujibu swali watapata marks nyingi kuliko aliyeandika kidogo. Si lolote si chochote; it's all because of poor writing skills!!!

Anicetus said...

We we anonymous una maisha ya upweke na ni mvivu was kusoma na kuandiaka..mery Xmas na heri ya mwaka mpya: Feliz navidad

Anonymous said...

ahsante sana hajj kwa kutupa kheir ya krismas na ndio mdau hapo juu kuna haja ya yote haya kumbuka jamaa ni mwenyekiti wa watanzania wote wa new York so lakiza akikuwish lazima asema na mambo ya jumuiya yake.

Anonymous said...

Mdau hapo juu kuhusu "haja ya maneno mengi"?. Don't be trivia and small minded. Hii ndio shida yetu waswahili. Tunakosa hata hulka ya kuheshimu the spirit with which something is said or done.

At this time and season of well wishing couldn't you for once keep your dirty mouth shut?

Anonymous said...

Tunataka ripoti kamili sio fupi ya matumizi ya fedha

Anonymous said...

Asante Ndugu mwenyekiti. Endelea na kazi yako mzuri. Huyo ni mlalamikajo tu.

Anicetus said...

Complete financial report is available to active members.